Mchipuko

MCA wa nakuru county Karanja Mburu apata ajali na kuaga dunia

Kulingana na mjibu wa habari ajali hiyo ilitokea asubuhi ya kuamkia leo karibu na viewpoint ndani ya gilgil nakuru katika barabara ya naivasha. Karanja Mburu alikuwa anaelekea nakuru kabla ya ajali kufanyika

Karanja Mburu ambaye ni MCA wa Lakeview ward alipoteza mwelekeo na gari lake kugonga mti uliokuwa kando ya barabara.

Samuel tanui ambaye ni naibu wa spika county ya Nakuru amesema mwili wa MCA huyo ulipatikana eneo la ajali asubuhi ya leo gari yake ikiwa imepinduka. Naibu wa spika alisema hawangeweza kujua ile ajali ilitokea saa ngapi.

Mwili wake uliweza kutolewa katika eneo la ajali na kupelekwa katika chumba Cha kuhifadhia maiti Cha Umash kilichoko Nakuru.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *