Mchipuko

Album ya Harmonize mbovu! Baba Levo asema

Bila uoga wowote, Baba levo amesema kuwa Album ya harmonize mbovu. Amesema kuwa amepata mda wa kuisikiza na hajaona ukali wowote

Kulingana na baba Levo, album ya harmonize ameipea asilimia kumi na nne. Akifananisha Album ya harmonize na ya Alikiba, Baba levo amedai kwamba afadhali ya Alikiba.

Album ya Alikiba ameipa asilimia tisini ila akasema Alikiba huwa haekezi kwa mziki. Kulingana na baba Levo, lazima marketing iwepo kwa kila biashara ya mziki ikiwemo. Amepeana Mfano wa boss wake diamond platnumz ambaye ameekeza sana kwa album yake inayotegemewa kuachiliwa mda wowote kuanzia Leo.

Baba levo amemshauri harmonize asiendelee na kutumia hela zaidi ku promote album hiyo na kutaka harmonize arudi studio akafanye album nyengine mpya.

Baba levo ni msanii na pia mtangazaji ambaye haogopi kuongea ukweli kuhusu msanii yeyote ule. Baba levo alisema hata diamond platnumz ambaye ni boss wake hana ruhusa ya kumkataza kuongea ukweli.

Akiongelea kuhusu album ya diamond platnumz ambaye inastahili kuachika hivi karibuni, baba levo alisema itakuwa kubwa sana kwani amepata nafasi ya kusikiza baadhi ya nyimbo.

Hapa mwangaza news yetu ni jicho tu huku tukingoja album mpya ya diamond platnumz. Tunatarajia album hiyo haitakuwa imejazwa amapiano tupu ila diamond platnumz ni msanii ambaye haendi na upepo.

Sikiza hii hapa: harmonize na Ibraah

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *