MchipukoSanaa

Alichokisema diamond kwenye uzinduzi wa label ya Rayvanny; Next Level

Alichokisema diamond kwenye uzinduzi wa label ya Rayvanny; Next Level Music

Msanii kutoka nchini Tanzania kwa majina Raymond shaban Mwakyusu ama ukipenda Rayvanny amefungua label yake ya music kwa jina “Next Level Music”. Rayvanny ambaye ana miaka 26 amekuwa kwenye label ya wasafi (WCB). Nyimbo zake tajika ni Kama vile Tetema, Natafuta kiki, zezeta na zinginezo.

Diamond platnumz amesema kwamba anamuunga mkono rayvanny kwa juhudi zake huku akiongezea kuwa atamsaidia ili kutimiza ndoto zake. Diamond amesema label ya rayvanny imefunguliwa kwa nia nzuri na kwa sababu hiyo itaweza kufanya vyema.

Diamond amesema kuwa tanzania kuna wasanii wengi wenye kipaji ila hawapati nafasi hivyo kumpongeza rayvanny ikizingatiwa nia ya label ya rayvanny ni kuwasaidia wasanii kama hao

Rayvanny atakuwa msanii wa pili kuwa na label yake baada ya harmonize kutoka wasafi na kuamua kuanzisha label yake ya konde gang. Tofauti ya hawa wawili ni kwamba, rayvanny ameanzisha label yake akiwa bado yupo WCB ila harmonize alijitoa kabisa kwenye label ya wasafi.

Rayvanny naye alionekana mwenye furaha kwani hii imekuwa ndoto yake na imeshatimia.

” Nachukua nafasi hii kuwaalika kaka zangu na dada zangu tufurahike pamoja ili kuzindua label yangu ya next level music”

Rayvanny aliwatembeza waliohudhuria ndani ya studio yake huku akiwaonyesha sehemu tofauti tofauti, muundo wa label yake mpya na mengi zaidi. Kujulikana kwa Rayvanny ilikuwa ni kupitia diamond platnumz mwaka wa 2015 alipomchukua kama mmoja wa wasanii wa label ya wasafi.

Kama umekuwa ukifuatilia mziki utakubaliana na Mimi kuwa wasafi ni mojawapo ya label kubwa afrika kwa jumla. Diamond platnumz amekuwa boss wake kwa miaka mingi na kama unakumbuka, kwetu ilikuwa nyimbo ya Rayvanny ya kwanza ambayo kwa youtube ipo na views zaidi ya million saba.

Soma hii pia ( Lavalava afunguka mazito anayoyapitia ndani ya wasafi label)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *