Mchipuko

Anjella atimuliwa na Harmonize na kutakiwa kulipa gharama ya bilioni

Habari za Anjella kutimuliwa ziligonga vichwa vya habari baada ya harmonize kujitokeza wazi na kutangaza kwamba Anjella hayupo tena kwenye Lebo ya konde music. Kwa wale wasiofahamu nyimbo za Anjella, aliwahi kufanya kolabo na Harmonize nyimbo kadhaa na Kati ya nyimbo hizo, “Kama” ilipata umaarufu zaidi mpaka wa Leo.

Wengi mnamfahamu msanii huyu wa kike ambaye sauti yake ni Ile watu husema hutoa nyoka pangoni. Msanii huyu kwa jina anjella amepatikana na changamoto baada ya kutolewa kwenye kisosi Cha Konde music world wide.

Kama unakumbuka vizuri harmonize alimchukua anjella kutoka kwa babake na kuahidi kumsaidia kimziki na pia matibabu kwani anjella ana tatizo kwenye mguu wake mmoja.

Sababu ya kufurushwa ndani ya konde music haijajulikana ila anatakiwa kulipa shilingi bilioni moja ya Tanzania ili aweze kuzipata digital platforms zote zake kama vile YouTube na zinginezo.

Kulingana na harmonize, amemuachia anjella huru na anadai kuwa yeye kashafanya yake na hapo ndipo amefika Kikomo kwa swala nzima la msanii huyu. Harmonize ambaye ndiye kiongozi wa konde music amesema kuwa anashangazwa na wengi kwa hatua aliyoichukua kwani watu wengi ikiwemo wapinzani wake  wanamuongelea vibaya na wakati yeye alikuwa akimsaidia anjella hawakuwahi msifia.

Ametoa mfano ulio wazi kwamba anjella amekuwa kama dadake na Kwa wakati amekuwa naye hakuhitaji chochote kimapenzi kama wengine wanavyofanya.

Bila shaka alikuwa anaongelea diamond platinumz na zuchu kwani zuchu alishindwa kukaa kimya na kumjibu harmonize. Kwenye insta story, zuchu alimshauri Harmonize kuwa afadhali angekaa kimya aweze kustiriwa kwani haya yote aliyataka mwenyewe.

Tutazidi kukupatia ripoti kamili kuhusiana na haya mpya Kati ya harmonize na anjella. Zidi kufuatilia habari zetu za mwangaza news.

Pia unaweza soma: Historia ya Anjella

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *