Mchipuko

Baada ya milele fm, jalang’o atangaza radio atakayojiunga nayo

Kusema kweli jalang’o amepitia mengi sana mwaka huu. Kama unakumbuka vizuri aliwahi kuhusishwa na kikundi flani Cha wanaume kinachosemekana hutumia wanawake kwa manufaa yao. Mwaka wa 2020 kwa kweli umekuwa mgumu kwake kwani pia ndio mwaka amepoteza kazi Kama mtangazaji wa milele fm.

Ni juzi tu gwiji huyu alitangaza kufungua station ya tv kwa jina jalango Tv ila itakuwa tofauti na tv zingine kwani tv yake itapatikana kwa YouTube channel.

Kuhusiana na malengo yake ya baadae, jalango aliahidi wakenya watarajie kitu kikubwa chenye pia kitanufaisha wanahabari na watangazaji wenza kwani wengi watapata nafasi ya kazi.

“YouTube channel yangu yaendelea vizuri na nashukuru sapoti yenu. Nataka nizidi kuikuza hii channel. Nafikiria pia niongeze vitengo tofauti Kama vile vichekesho, michezo, habari na mengi zaidi. Nina Imani nikifanya hayo yote wengi watapata kazi.

Tangu jalang’o aondoke milele fm, wengi wamekuwa wakiulizia radio atakayo jiunga nayo. Hivi maajuzi alitangaza kuwa amepata radio karibia sita zinazotaka afanye kazi na wao ila bado hajafanya maamuzi.

Juzi katika channel yake ya YouTube, jalango alijaribu kuongelea hili swala kuhusiana na maisha yake ya baadae na alikuwa na haya ya kusema;

” Najua kila mtu anataka kujua mipango yangu ya baadae, kwanza kabisa sitafanya kazi milele fm. Najua kila mtu anajiuliza maswali mengi kunihusu radio nitakayojiunga nayo..”

Kulingana na jalang’o, milele fm ndio alitaka iwe radio ya mwisho kwake kufanya kazi. Ina maana kuustaafu kwake kumevutwa karibu maana kwa sasa hayupo kazini tena.

” Nasikitika maana nilitaka kumaliza Safari yangu Kama radio presenter ila naona Safari yangu imekatika mapema. Nilifikiria nitafanya kazi milele fm mpaka kuustaafu kwangu. Kulingana na mimi, sikutaka kuacha kazi ndani ya milele fm ila sina la kufanya…

Kulingana na maongezi yake, jalang’o huenda akajiunga na radio Africa kwani wao wanaweza kumlipa hela anazozitaka.

” Leo pia nimepokea simu ya nane kutoka kwa mwenzangu Bonni Msambi anayefanya kazi KBC na kuniulizia mipango yangu. Alitaka sana tufanye kazi pamoja ila nikakwambia siwezi maana yeye mwenyewe anafanya kazi nzuri tayari. Huenda nikajikuta waiyaki way ambapo kuna radio kadhaa Kama vile kiss FM, NRG, Radio Jambo, classic Fm…..”

Soma hii pia (Mengi kuhusu azziad Nasenya)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *