Mchipuko

Babu Owino azidi kukashifiwa kwa kitendo alichofanyia dj Evolve

Mbunge wa Embakasi Babu Owino anaendelea kupitia wakati mgumu baada ya wakenya kuzidi kumkashifu kwa kitendo alichofanyia dj Evolve. Ni Kama miezi sita saa baada ya Mheshimiwa Babu Owino kuhusika na tendo la kumpiga risasi na kumjeruhi DJ Evolve.

DJ Evolve shot

Tendo hili likifanyika ndani ya club moja jijini Nairobi ambapo DJ Evolve hufanyia kazi yake. Babu Owino aliweza kumpeleka hospitali na tangu siku hiyo, DJ Evolve amekuwa hospitalini takriban miezi sita.

Kulingana na familia ya dj Evolve, bill ya hospitali imefikia million kumi na saba ambapo yadaiwa Babu Owino amelipa kiwango flani japo aliahidi kulipa pesa yote. Kwa sasa hawezi kutembea na anahitaji huduma maana hakuna anachoweza kukufanyia mwenyewe.

DJ Evolve in club

Siku ya jumatatu, DJ Evolve aliweza kufanya mazungumuzo na runinga ya NTV na alionekana mnyonge kiwango kwamba hata kuongea kwake ni shida. Mamake alieleza kuwa hajawahi kuongea na Babu owino lakini anaomba mahakama iweze kumchukulia hatua kwani anachokipitia mwanawe mungu tu ndiye anajua.

Kuanzia Jana, wakenya wameungana na kutaka hatua ichukuliwe huku wakionekana kutoelewa ni lolkwa Nini Babu Owino ako huru ikizingatiwa kuwa kila mtu aliona alichokitenda kupitia video ya CCTv.

Babu Owino DJ Evolve

Huko twitter kuliwaka moto kila mmoja akilaumu mkono wa Sheria kwa kukawia kumchukulia hatia mheshimiwa Babu Owino.

DJ Evolve na babu Owino

migunamiguna on twitter babu Owino DJ Evolve DJ Evolve death

Hapa mwangaza news tunafuatilia haya matukio na tutazidi kukujuza zaidi. Usisahau kubofya kengele nyekundu ilioko pale chini pembeni upande wa kulia ili usipitwe na habari zetu.

Soma hii pia (afya ya Raila odinga)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *