Sanaa

Barua rasmi kwa Coronavirus

Shikamoo,. Natumai hii barua itakufikia kivyovyote vile. Mwanzo kusikia kuhusu wewe ilikuwa ni Kama miezi mnne iliyopita huko nchini china. Nilifikiria labda utakaa kwa mda alafu utarudi kwenu lakini naona niliwaza visivyo. Pia sikufikiria kuwa ungefika kwetu nilidhani utabakia humo china.

Kutoka uje umehangaisha nchi nyingi sana na Hali sio Hali kwani umefanya hata wanainchi hawana Uhuru kabisa. Wengi wameacha kwenda makwao kazini wakikuhofia kwani hauna huruma kabisa mpaka imefikia hatua unaua.

Shule siku hizi zimefungwa na watoto tunaowategemea wawe viongozi wa kesho wanakesha nyumbani wakitazama unavyohangaisha dunia nzima. Wazazi wameishiwa kabisa mpaka imekuwa vigumu kulisha familia sababu hawako kazini na mapato hakuna. Swali ni, wataka Nini?

Tumesahau hata salamu maana hauruhusu utumiaji wa mikono. Siku hizi twaonekana Kama tumekosa nidhamu maana hatuamkui watu na mikono. Imekuwa vigumu kutoka sehemu moja au nyengine ina maana hatuwezi kutengamana hata na familia zetu za mbali.

Maisha yetu yamebadilika na hivi karibuni tutakosa hata chakula. Madaktari wanafanya juhudi ili kukuangamiza lakini umekita kambi huku ukijipiga kifua na kuonesha wazi hutaki kutoka. Coronavirus, tulikukosea Nini?. Huna dawa kabisa hata hatuwezi kukuzuia. Umeamua kutuangamiza bila hata sisi kukukosea. Kila mmoja anajiuliza, Nani alikutuma? Hivi, waweza ukatuacha na amani?

Soma hii pia Habari( nzuri kutoka china)

Hatukuoni Ina maana kupigana na wewe itakuwa kazi ngumu. Kama tumekukosea tunaomba msamaha na uachane na maisha yetu.

Ni Mimi wako mwanainchi

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *