MaishaMchipuko

Ben Kitili, mtangazaji KTN TV, na Amina waachana

Mtangazaji wa KTN Ben Kitili ameachana na mke wake Amina mude. Wawili hawa wameachana miaka miwili baada ya kufunga pingu zao za maisha.

Kwa Instagram yake, mke wa Kitili alitangaza huku akieka kumbukumbu yao katika harusi yao bila kusahau kumbukumbu ya watoto wao.

Ben Kitili wife and children

Amina mude alisema anapitia mengi. Tofauti zao zilianza mwezi mmoja uliopita na kwa sasa hajafanya maamuzi ya maisha yake ya baadae. Aliweza kufuta picha zote za Bwanake Ben Kitili zenye zilikuwa kwa Instagram page yake.

Kulingana na Amina, kuachana kwao hakutazuia malezi ya watoto wao ila wawili hawa watashirikiana kwa chochote kile ili watoto wao wapate malezi bora.

Ben Kitili wife Amina mude wedding

Walifunga pingu zao za maisha katika hoteli moja Nairobi baada ya wachache kupata mwaliko. Wengi walianza kukashifu Amina kwa kufunga ndoa na mkristo ila hilo halikumfanya abadilishe nia yake ya kuwa na Ben Kitili.

“Katika ndoa, Mungu ni mkubwa kuliko dini, kwa wale wote hawajafurahia maamuzi yetu tunawasamehe. Una ruhusiwa kufanya utakacho ila sio kuingilia maisha ya wengine….Kitili aliyasema haya.

Mwaka uliopita, wawili hawa walifanikiwa na mtoto wao wa pili mvulana kwa jina Roman hami Kitili.

Soma hii pia ( afya ya Raila odinga)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *