Maisha

Betty Kyalo aelezea aina ya mwanaume anayemtaka kuzaa naye

Baada ya kuacha kazi K24, Betty Kyalo anaonekana kufichua siri nyingi kumhusu. Mengi sana ameyaweka wazi katika channel yake ya youtube. Kwa sasa Mwanadada huyu ako “Single” na inaonekana ako tayari kuingia kwenye uhusiano upya.

Betty Kyalo hataki mwanume wa kawaida ila kulingana na yeye, angependa kuwa na uhusuano na mwanaume mwenye ameachwa ama ameacha mkewe… Makubwa haya!….Nafikiri kinachochangia uamuzi wake ni kuwa yeye pia aliachika kwa hivyo huenda akaelewana bora zaidi na mtu aliyeachwa pia.

Kwa sasa amesema bidii yake ya kikazi ni kwa sababu ya mtoto wake. Amekili kuwa yeye hana “Sponsor” kama wengi wanavyodhania ila anafanya bidii ili maisha ya mtoto wake yawe sawa hapo mbeleni. Kulingana na yeye, maisha ya mtoto wake wa kike ni mhimu hata kuliko yake. Aliongezea na kusema mda ukifika ataongeza mtoto mwingine.

Aliweza kusema makosa aliyoyafanya kwani kulingana na yeye alifanya uamuzi mbaya wa kuolewa mapema.

“…..Mwanaume mwenye ameachwa na mkewe atakupenda kwa dhati kwani atajaribu kuziba pengo lililoachwa na mkewe ila mwanaume mpya atahitaji mambo mengi kutoka kwangu kama vile kupikiwa na mimi na itakuwa vigumu maana kazi zangu zafanyika hata usiku wa saa nne kumanisha nitachelewa kuingia nyumbani mara nyingi…..”

Soma hii pia (Kutana nao wanawake warembo Ukambani)

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *