MaishaMchipuko

Betty Kyalo : Niko tayari kuolewa tena

Mtangazaji wa station ya K24 Betty kyalo amesema ako tayari kuolewa tena. Kama unakumbuka vizuri kipusa huu alikuwa mkewe Dennis Okari ambaye ni mtangazaji NTV. wawili hawa waliweza kufanya harusi ya kifahari ila uhusiano wao ulikatika hata kabla ya mwaka mmoja kuisha.

Katika account yake ya Instagram, Betty Kyalo amewaeleza wafuasi wake kwamba ashaelewa makosa yaliyofanyika na yuko tayari kurudi kwa uhusiano. Kwa mda mrefu Betty Kyalo alikata tamaa ya kuwa kwa uhusiano baada ya talaka yake na Deniss Okari. Ameongezea kusema saa hii yuko tayari kutulia na hivi sasa anamtafuta atakaye funga naye pingu za maisha.

Kama unakumbuka vizuri, mwana habari huyu ashawahi kuhusishwa na Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho na wengi walidhania wawili hawa wako kwenye uhusiano wa kimapenzi. Alipoulizwa kuhusu taarifa hii alikana kabisa akidai kuwa yeye na Joho ni marafiki wa kawaida.

Alipoulizwa kuwa kama anna mazungumuzo na wanaume wake wa zamani, Betty Kyalo alisema huwa anaongea nao ila hayuko tayari kurudiana na yeyote ule.

Soma hii pia ( Kutana na wanawake warembo kutoka Ukambani )

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *