Burna boy awabwaga diamond platnumz na Wizkid kwenye tuzo za BET Awards 2021
BET awards 2021 zimefanyika na tunaweza sema tuna washindi kutoka ulimwengu mzima.
Gwiji Burna Boy kutoka Nigeria ambaye majina yake kamili ni Damini Ebunoluwa Ogulu amekuwa mshindi wa 2021 Best international act ndani ya BET awards.
Bali na diamond na Wizkid, wengine aliowashinda ni pamoja na Aya Nakamura kutoka France, Emicida kutoka Brazil, Headie one kutoka UK, Young T & Bugsey pia kutoka UK na Youssoupha kutoka france pia.
Hii ni Mara ya tatu ya Burna Boy kunyakuwa tuzo la Best international act BET Awards. Mara ya kwanza alishinda 2019, 2020 na huu mwaka wa 2021.
March 2021, Burna Boy alikuwa msanii wa kwanza Nigeria kushinda Grammy kupitia album yake ya twice tall. Hii ilikuwa Grammy awards ya 63. Kumbuka Grammy hufanyika kila mwaka.
Katika afrika mashariki, diamond platnumz ndiye msanii wa kipekee aliyewakilisha 2021 BET Awards.
Mwaka wa 2017, Rayvanny alikuwa msanii wa kwanza kushinda baada ya kuchaguliwa kama the best viewers choice best new international act. Hii ilimfanya awe msanii wa pili kuwa mshindi wa BET awards kwani Eddy Kenzo aliwahi kuwa mshindi wa international viewers award mwaka wa 2015
Ni tuzo zilizokuwa zimengonjewa sana kwani zilizua gumzo kwenye mitandao wengi wakiulizana kama Diamond platnumz angeweza kuwashinda haya magwiji wa nigeria.
Kufutia kuteleuliwa kwa diamond platnumz kuwania tuzo za BET, kulizuka mgawanyiko na sio wote waliamua kumpigia Kura Diamond platnumz kwa madai tofauti.
Kuna watanzania wengine waligoma hata kumpigia Kura Diamond wakidai siku hizi ana maringo Ila wengine walimpa sapoti wakidai Diamond angeshinda hizo tuzo ingekuwa sifa kwa taifa la Tanzania ndipo wakahimiza waliogoma kumpigia Kura wampigie Kura kwa niamba ya taifa lao.
Hapa mwangaza news tunampongeza diamond platnumz kwani hata kama hakushinda h izo tuzo, aliwakilisha afrika mashariki maana hata kuteuliwa kuwania hizo tuzo pia ni Jambo kubwa sana.