Mchipuko

Chanzo Cha kifo cha Rais Pierre Nkrunziza

Rais wa Burundi Pierre Nkrunziza amefariki dunia Leo akiwa na umri wa miaka hamsini na tano.

Ripoti zinasema kuwa rais Pierre Nkrunziza alifariki ndani ya hospitali ya karusi fiftieth anniversary chanzo ikiwa ni ugonjwa wa moyo. Kifo chake kilitokea tarehe nane June mwaka wa 2020.

Jumamosi alikuwa yuatazama volleyball sehemu inayojulikana Kama ngozi ila usiku ndio akaanza tatizo. Alikimbizwa hospitalini na hali yake ya ki afya ilikuwa imeanza kuwa sawa. Hata aliweza kuongea na watu Waliokuwa karibu na yeye.

Pierre Nkrunziza

Burundi ni nchi ya pekee yenye haikusitisha michezo wakati huu wa janga la Coronavirus. Juzi tu nchi ya Burundi waliweza kufanya uchaguzi ambapo general Evariste Ndayishimiye alipata ushindi na asilimia 69 za kula zote zilizopigwa.

Hali ya ki afya ya rais Nkrunziza ilianza kuzorota siku ya jumatatu. Madaktari walijaribu juhudi zote ila hawakufaulu.

Burundi wamepoteza rais aliyekuwa mzalendo. Alikuwa mcha mungu. Serikali ya Burundi wametangaza siku saba za matanga na bendera itafungwa nusu mlingoti.

Juzijuzi Nkrunziza alitishiwa na shirika la afya duniani kwani alionekana kupuuza kupigana na maambukizi ya coronavirus. Mwezi uliopita aliweza kuwafukuza wasimamizi wa kuzuia maambukizi ya coronavirus wa kituo Cha afya Cha WHO. Aliwaagiza watoka nchini Burundi na warudi kwao. Mkewe Nkrunziza, Denise Bucumi ako aga Khan university hospital nchini Kenya akiwa na ugonjwa wa Coronavirus

Ripoti zinasema Mrs. Nkrunziza aliletwa Nairobi kutoka Bujumbura kutumia ndege ya AMREF. Kwa sasa hali yake haijulikani iko vipi.

Kesi za corona nchini Burundi ni 83 huku mtu mmoja ndiye aliyelipotiwa kupoteza maisha.

Soma hii pia ( utajiri wa Ruto)

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *