Mchipuko

Coca-cola girl :Wakenya wazidi kuisukuma kampuni ya coca-cola

Kama wewe ni mtu wa kufuatilia mitandao, basi utakuwa umekutana na huyu msichana ambaye kwa sasa amebatizwa jina la Coca-cola girl. Msichana huyu ametokea county ya baringo na kusema kweli ipo kila sababu ya kumsaidia kwani picha zake zimeenea kila sehemu.

Jebiwott ambaye ndio jina lake kamili alipiga picha  akiwa amevalia nguo za kiasili huku akiwa ameikamata chupa ya soda ya coca-cola. Coca-cola girl ama ukipenda Jebiwott anaelewa sana mambo ya picha na tabasamu lake ni la kikweli. Mpiga picha kwa jina Daggy shy hakujua itafikia hapa ila kwa sasa kazi yake inaonekana ulimwengu mzima. Sio picha moja tu mbali mtoto huyu ana picha zaidi na tofauti zinazoonyesha asilia.

Coca-cola girl

Kulingana na babu yake Jacob Keror, zoezi hili lote la picha liliweza kufanyika nyumbani mwa nyanyake Coca-cola girl huko Eldama Ravine. Wakenya katika sehemu mbalimbali wamejaribu ku share picha za Jebiwott huku wakiitaka kampuni ya Coca cola kumpa mtoto huyu kazi ya matangazo. Haikufikia hapo, kuna mkenya mmoja aliamua kumaliza kazi yenye ilitakiwa kampuni ya cocacola kuifanya na kuamua kutengeneza tangazo la ccoca cola akitumia picha za Jebiwott

Coca-cola girl

Kulingana na utafiti wetu, huenda ikawa vigumu sana kwa mtoto huyu kufanya matangazo ya coca cola kwani pia wako na sheria zao. Kampuni hii kumpa kazi ya matangazo mtoto mwenye ako chini ya miaka kumi na mbili ni kinyume na sheria zao.

 

Hapa ndani ya mwangaza news tunaiomba kampuni tajika iweze kufanya chochote kile kwa mtoto huyu kwani picha zake zimeiletea sifa kampuni hii na sio kenya tu ila ulimwengu mzima kwa jumla.

Soma hii pia ( Mengi kuhusiana na Azziad na ringtone)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *