Afya

Coronavirus ni nini na kwanini ni hatari.

Wengi wanafahamu ugonjwa huu lakini sio wengi wanaolewa kwa undani zaidi Coronavirus ni nini. Kwa Sasa ugonjwa huu umeua wengi sana na wengi wako hospitalini wakipokea matibabu.

Coronavirus ni nini?

Ni Aina ya maswali wengi wetu tunajiuliza Ila nitakupa jibu kwa sasa.Ni  aina ya kirusi mfano wa ufuta ambapo kiingia kwa mwili wako, kinakula viini vinavyoleta Kinga mwilini hivyo kuhatarisha afya yako na kukuwacha kwa hatari ya kupata maambukizi. Kirusi hichi kinajulikana Kama covid-19 ama Sars-coV9.

Nini inafanyika kwa mwili ukiwa na Coronavirus?

Kiwango cha virusi utakachoambukizwa ndicho kitakachopigana na mfumo  wa Kinga ya mwili wako, Ina maana Kama virusi ni vingi Basi mfumo wa Kinga ya mwili wako utakuwa na kazi nyingi ya kupigana na na virusi vya covid-19.

Wakati unapopata virusi hivi Basi utakuwa katika harakati za kusambaza virusi hivyo kwani zinabakia katika upande wa juu wa kupumua ikiwa ni kwenye Koo na pua.

Wakati mgonjwa wa Coronavirus anapopumua ama kukohoa huwa anasambaza virusi na huenda zikampata aliye karibu. Anapoongea mtu pia hutoa matone yanayobaki hewani na Kama itamrukia mtu mwingine basi atakuwa ashapata virusi. Hii ndio sababu kuu ya kuelezwa na wasimamizi wa afya tuweze kuweka umbali wa mita moja na wenzetu tunapotengamana. Bado hakijajulikana wazi unafaa kupata chembechembe ngapi kwa mwili wako ili uanze kuungua.

Tunahimizwa tuweze kuosha mikono yetu kila Mara ili kujikinga na maambukizi. Pia ni vizuri kuwa na barakoa (mask) ili tuweze kujizui na kuzuia wenzetu kutokana na maambukizi.

Coronavirus ni Nini

Wahudumu wa afya wako kwenye hatari ya kuambukizwa kwani Mara nyingi wanatengamana na wagonjwa wa homa ya Coronavirus. Inasemekana Kati ya watu kumi na mbili waliombukizwa Coronavirus, wanne wao ni wahudumu wa afya. Nchini Italia, Spain na china asilimia ishirini na tano waliopoteza maisha yao ni wahudumu wa afya.

Kwa taarifa hiyo najua umejifunza mengi kuhusu Corona na umeelewa vizuri Coronavirus ni nini. Asante kwa kuendelea kufuatilia habari zetu za mwangaza news. Waliofanikisha habari hizi ni pamoja na kituo Cha BBC.

Hii habari ikikupendeza zaidi fanya Kama una share na wenzako kwa kubofya Facebook ama Tweeter icon hapa chini

 

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *