MaishaMchipuko

Fahyvanny aongea mazito kuhusu Rayvanny

Ni kweli wawili wapendanao hata wakiachana usiwahi ingilia na Kuna msemo unasema wawili waliotumia shuka moja wanajua Siri zao wenyewe.

Hii imeonekana wazi kwake fahyvanny kwani kwa sasa bado anonekana kumzimia aliyekuwa mume wake wa hapo awali, Rayvanny. Huenda wawili hawa watakuja kuwa pamoja japo wote wanadai mapenzi yao yaliisha.

Fahyvanny na Paula

Paula na Rayvanny

Fahyvanny kwa upande wake anasema hana chuki na Paula Kajala hata washawahi kuongea kwa Mara nyingi. Paula Kuna mda aliwahi kumpigia simu fahyvanny akitaka bidhaa Fulani na wakaelewana atamtafutia.

Baada ya bidhaa hizo kupatikana fahyvanny alimpigia Paula simu ila bei ikamzidia Paula na kusema atanunua wakati mwingine.

Kuna mda fahyvanny aliwahi kuulizwa kama anaweza Kubali Paula aishi na mtoto wake ila akakataa kabisa.

Fahyvanny na Rayvanny

picha za fahyvanny na Rayvanny

Kulingana na utafiti wetu, fahyvanny bado anampenda Rayvanny japo anasema yeye na Rayvanny ni marafiki na wazazi na kinachowaleta karibu ni mtoto waliozaa pamoja. Kinachoshangaza watu ni, Kwanini fahyvanny hajaamua kutafuta mpenzi mpya na aendelea na maisha yake.

Upande wa Rayvanny anaonekana “ku move on” kwani saa hii anamiliki Paula ambaye ni mwanawe kajala masanja.

Fahyvanny kwenye mahojiano na wasafi media alisema hajutii Rayvanny kuchuliwa na Paula huku akisema labda ni mipango yake Mungu na huenda alikuwa anamuepusha na Jambo mbaya ambalo lingekuja tokea kama wawili hawa wangeendelea kuwa pamoja.

Fahyvanny aliongeza kusema kwamba, kuwa single kwake haimanishi bado anataka warudiane na Rayvanny ila ni kwa sababu hajapata mwanaume mwenye anaweza kumfaa. Amesema wanaume wengi wamekuwa wakimtongoza. Kunao wengine wanawatuma na marafiki wa fahyvanny  lakini bado hajapata mwanaume ambaye anaweza kufunga naye pingu za maisha.

Rayvanny na fahyvanny

Kulingana na fahyvanny, kama Mungu amewapangia kuwa siku moja warudiana basi yeye hatapinga na Yuko tayari ila kama sio mapenzi yake Mwenyezi Mungu, basi watabaki kuwa marafiki ama wazazi ili waweze kumlea mtoto wao.

Rayvanny anaonekana kuendelea na maisha yake na kwa sasa ametosheka na Paula. Kulingana na yeye, hawezi Kubali kuongea vibaya kuhusu fahyvanny kwani yeye ni mama wa mtoto wake na anampa heshima kama mzazi mwenza.

Hapa mwangaza tunazidi kuwafuatilia watatu hawa na chochote kikitokea tutakuwa wa kwanza kuwajuliza. Endeleeni kufuatilia habari zetu hapa mwangaza news kwa habari kamili.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *