SanaaMaisha

Firirinda yake dick wanyonyi yasifiwa na Ezekiel Mutua

– wimbo huu wa Firirinda umejulikana na wengi baada ya miaka 35 tangu uliporekodiwa

– Firirinda imesifiwa na Kenya film board kwa kusemekana kuwa wimbo mzuri usiokuwa na matusi na unaonyesha utamanduni.

– Nyimbo hii ya Firirinda imeacha watu hoi na kila mtu kwa mitandao anaonekana kufurahia wengi wakijaribu kuucheza kwa kile wanachokiita Firirinda dance challenge.

Dick Munyonyi alirekodi wimbo huu miaka 35 iliyopita. Kwa maajabu, wimbo huu wa Firirinda umekuja kugonga vichwa vya habari mwaka wa 2021. Najua hii imemshangaza sana msanii huyu na sidhani kama alifikiria kuwa wimbo huu ungekuwa mkubwa baada ya miaka hiyo yote.

Kwa mda wa wiki moja, wimbo huu ume trend kwa mitandao kama vile tiktok, facebook, whatsapp. Hivi majuzi Ezekiel mutua ambaye anasimamia KFCB alisifia sana wimbo huu huku akisema unaonyesha heshima. Ezekiel Mutua amewaomba vijana kuachana na nyimbo zenye hazina heshima na kurekodi nyimbo kama Firirinda.

Kulingana na ezekiel Mutua, Firirinda inaweza kusikizwa na watu wote lakini nyimbo wanazorekodi vijana ni za aibu kwani sio nyimbo za kusikizwa na watu wazima. Baadhi ya mistari kwenye hii nyimbo inasema… “wageni wapikiwe chai na wenye hawatumii chai wapewe chai bila Sukari. Jina Firirinda imetokana ” Free Rinda” nguo zinazovaliwa na wanawake na kuwawezesha kucheza vizuri.

Tazama wakenya wakicheza Firirinda

Wanainchi wamemuomba Ezekiel mutua kumsaidia Dick wanyonyi ambaye bado anaugua na anahitaji matibabu.

Dick wanyonyi aliachana na usanii baada ya kupata ugonjwa wa T.B ( tuberculosis). Ugonjwa huu ulifanya sauti yake kuharibika hivyo kuwa vigumu kwake kuweza kuimba tena. Kwa sasa bado anaendelea na matibabu na kila mwezi anatumia Elfu tatu za dawa. Mkewe naye anaugua ugonjwa wa Sukari ambaye naye Kila mwezi anahitaji Elfu mbili za hospitali.

Soma hii ( mwanamke amuua mwanawe kwa kumchinja)

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *