Sanaa

Gates mgenge arudi radioni, je atasaidia sanaa ya pwani?

Ni kipenzi Cha mashabiki wengi sana japo wasanii wengi hapa mkoani pwani hawampendi kwa kile wanakiita mapendeleo. Gates mbali na presenter, ni m.c mkali sana na sherehe nyingi huongozwa na bingwa huyu.

Gates alisimamishwa kazi pamoja na wenzake miezi kadhaa iliyopita baada ya radio alimokuwa kufanyiwa mabadiliko yaliyochangia kupoteza kazi kwa watangazaji kadhaa akiwemo.

Kama umekuwa ukifuatilia bingwa huyu utakubaliana nami kuwa Ana uzoefu mkubwa sana na akiwa kwenye radio humakinika zaidi na huvutia mashabiki wengi sana.

soma ( Selina na pete yazua gumzo)

Gates mgenge kwa sasa ako wapi?

Kwa Sasa yupo pwani FM alipoanzia  utangazaji. Hapa mwangaza tunamuombea kila la heri na mungu azidi kumfungulia njia zaidi. Mashabiki wake wengi wameweza kuandika meseji ya kumpongeza katika account zao za facebook huku wakisifia kazi zake na kudai kurudi kwake kutasaidia sana sanaa ya pwani

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *