Sanaa

Gumzo yazuka Kati ya mashabiki wa Selina na pete ndani ya maisha magic

Wakati huu ambapo wanainchi wanafanya kazi nyumbani, mnet imehakikisha inawapa burudani ya kukata na shoka ili kuhakikisha wakenya wanaendelea kupata burudani inayostahili.

Maisha magic na maisha magic plus wamehakikisha kuwa utaendelea kupata burudani na hivo kuongezea vipindi zaidi. Kovu,kina na tehanani ni baadhi ya vipindi mpya na bila shaka ni vipindi vilivyofanyiwa utayarishaji wa Hali ya juu.

Selina na pete ni vipindi vimekuwapo kwa mda Sasa na kusema kweli vimepata mashabiki wa kutosha. Miezi kadhaa iliyopita, tamthilia ya Selina ilieza kutunzwa Kama tamthilia Bora nchini Kenya huku Pascal anayejulikana Kama Nelson ndani ya Selina akichaguliwa kuwa muigizaji Bora wa kiume.

Kwa mda sasa, mashabiki wa Selina wanaonekana kukerwa na wanachokitaja kuwa maelekezi mabaya huku wakisema kiongozi wa tamthilia hii amepungukiwa na mawazo. Japo wengi wanasema kuwa uelekezi wa tamthilia hii ni mbaya, Selina bado inapata utazamaji mkubwa kuliko tamthilia zinginezo hapa nchini Kenya.

Pete ni tamthilia ya pili inayopata utazamaji mkubwa hapa nchini Kenya na Tanzania kwa jumla. Watanzania wamekuwa wakifuatilia tamthilia hii kwani muigizaji mkuu katika tamthilia hii ametokea nchini Tanzania. Kwa Sasa tamthilia hii inapata sifa tele na kusemekana kuongozwa ki umakini zaidi.

Yote Tisa, kumi ni kuwa tamthilia zote zinaleta burudani na ni kweli katika wakati huu wakenya wamo nyumbani, burudani inapatikana ya kutosha. Tunazidi kuwashukuru maisha magic na maisha magic plus kwa burudani.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *