Mchipuko

Hali tatanishi ya kilichomuua Ramadhan Kajembe

Aliyekuwa mbunge wa changamwe Ramadhan kajembe aliaaga dunia ijumaa. Hii ni baada ya kulazwa hospitali ya Pandya Memorial Hospital iliyooko Mombasa county kwa mda wa wiki mbili.

Mbunge wa jomvu twalib ambaye ni mmoja wa familia ya kajembe alisema marehemu alilazwa hospitalini mda mfupi baada ya mkewe kufariki.

Zaharia, mke wa pili wa Ramadhan kajembe alifariki wiki mbili zilizopita huku ikitangazwa kuwa alikufa kutokana na homa ya Covid-19. Familia ya kajembe imepitia mengi kwa mda mfupi kwani mke wake wa kwanza alifariki Kama miezi nne iliyopita.

mazishi ya Ramadhan Kajembe

Twalib alikanusha madai kuwa Ramadhan kajembe alifariki kutokana na virusi vya coronavirus

“Sisi sio madaktari na hatuwezi kusema marehemu amefariki kutokana na virusi vya coronavirus.. ufahamu wangu Ni kuwa marehemu alilazwa hapa kwa ugonjwa tofauti…”

Rais Uhuru Kenyatta kupitia twitter account, alimsifia mwenda zake Kama mtu mwenye bidii aliyetumikia nchi yake vizuri kwa miaka mingi. Naye naibu wa rais William Ruto hakuachwa nyuma kwani alimtambua marehemu Kama mtenda kazi aliyeyewasaidia Wana changamwe bila uoga wowote.

Wengine waliotuma rambirambi zao ni pamoja na gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho. Joho alisema Ramadhan kajembe alisimama na watu wake kwa kutetea wanainchi wa maeneo mbalimbali

ali Hassan Joho

Maisha ya Ramadhan Kajembe Kama mwanasiasa

Alipata ubunge wa changamwe mwaka wa 1997 na kutetea kiti hicho mwaka wa 2002 na 2007. Jina lake Ni tajika Mombasa nzima. Amekuwa mbunge kwa miaka thelathini. Alipoteza kiti Cha ubunge mwaka wa 2013 baada ya kushindwa na aliyekuwa senator wa Mombasa hassan Omar

Ramadhan Kajembe ashawahi kuwa mwenye kiti wa Kenya ferry services na pia ashawahi tumikia Mombasa municipal council

Mtoto wake Seif Kajembe aliwahi kuwania kiti Cha jomvu lakini alishinda na twalib aliyekuwa MCA wa Jomvu kuu

Soma hii pia ( hakuna corona nchini Tanzania)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *