MchipukoSanaa

Harmonize aangukia dili ya mamilioni

Baada yakutoka wasafi, inaonekana mambo yanamfungukia harmonize. Ni juzi tu alipomtambulisha msanii mpya ibra na huenda akaongezea wasanii zaidi. Wengi wanasema huenda akakwama Ila mambo yanavyokwenda ni Kama amejipanga zaidi na huenda akafanya maajabu zaidi.

Upande ule mwingine diamond platnumz amemtambulisha zuchu msanii wa kike ambaye ni mwanawe Khadija kopa. Hizi timu mbili zaonekana kuwa na mashindano makubwa sana na kila mmoja anajitahidi kivyovyote ili aonyeshe mwenzake ana uwezo zaidi.

Harmonize ameangukua dili ya CRDB bank

Harmonize ameangukua dili na benki moja nchini Tanzania na kuanzia hizi Sasa atakuwa anapokea mamilioni ya pesa kama balozi wa benki hiyo. Kwa Sasa hatujajua anapokea hela kiasi gani lakini Kulingana na kiwango Cha jina lake lazima iwe hela nyingi.

Bado tunazidi kufuatilia tokeo hili na kadri habari inavyozidi kuchipuka nasi tutazidi kukujuza kwa makini zaidi. Asante kwa kuwa mfuasi wa mwangaza news

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *