Mchipuko

Harmonize ameamua ku unfollow wasanii wote kwa Instagram page yake

Harmonize Instagram: Harmonize azidi kufanya vituko na kikubwa alichokifanya ni ku unfollow wasanii wakubwa wa Tanzania. Juzi Ali unfollow diamond platnumz  na wasanii wote wa WCB. Wengi walidhania labda ni beef zao ila Leo pia kaongeza orodha mpya.

Alio unfollow Leo ni pamoja na wasanii wa konde Gang wakiwemo Ibraah, killi, chidi, country boy  pamoja na Angela. Sababu yake aliyoitoa kutokana na uamuzi huo ni kwamba kwa sasa ana mpenzi mpya ambaye ndiye pekee anafaa ku follow ili aweze kumpenda zaidi.

Maswali mengi yamezuka wengi wakiulizana kwani mtu akiwa na mpenzi hafai ku follow mtu yeyote kwenye Instagram?. Hayo ni baadhi ya maswali ambayo mpaka sasa hatujapata majibu.

Instagram ya Harmonize

Kabla ya ku unfollow wasanii hao, harmonize alikuwa ana follow watu zaidi ya mia tisa ila kwa sasa ana follow watu mia mbili na kitu. Wasanii walioponea na bado ana wa follow ni Aslay, Jaydee pamoja na Mr Blue.

“I love everybody out there but I just wanna follow the woman of my life. So don’t feel like I don’t love you and respect you after unfollow you mean alot to me Life”

Hivi ndivyo alivyoandika kupitia insta story akitumia kizungu chake cha kutafutatafuta.

Hivi karibuni, harmonize na diamond platnumz wameonekana wakirushiana maneno kupitia Instagram page zao na anayesemekana kuanza ni diamond. Diamond platnumz aliandika kwa Instagram page yake kwamba wasanii wafanye bidii wasije wakaingia kwenye mihadarati.

Diamond platnumz aliendelea kumsifia Rayvanny kwa kupata nafasi ya ku perform katika MTV awards huku akisema kuwa wasanii wanafaa kuwa na fadhila na heshima Kwa wale waliowasaidia. Aliendelea kumkanya Rayvanny asiwe kama wasanii hao ambao hawana fadhila.

Harmonize aliona amelengwa yeye na akaamua kumjibu kupitia Instagram page yake na kusema. Kama ingekuwa lazima mtu alipe fadhila basi yeye atakuwa anadaiwa na Tanzania nzima.

Aliendelea kusema kuwa baba levo amelipwa ili amtukane lakini wenye wanamlipa wamesahau kwamba wanamlipia harmonize promotion na mziki wake utaendelea kujulikana zaidi kwani haufi Leo.

Mkikosa tuzo zisizonunulika msinune, kaeni msubiri Afrima.

Harmonize aliandika hivi kwani diamond platnumz hakupata tuzo ya MTv Jana. Diamond platnumz alikuwa ameteuliwa kwenye kipengele Cha msanii bora afrika ila Wizkid akawa mshindi.

Ni hayo tu Kwa Leo wacha tungoje mapya kutoka kwa wasanii hawa wanisemekana kuwa wasanii wakubwa Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *