Sanaa

Harusi ya diamond platnumz yanukia, tazama hapa

Diamond Platnumz ambaye kwa jina kamili Anajulikana Kama Naseeb Abdul ni mmoja Kati ya wasanii matajiri Tanzania na afrika kwa jumla. Msanii huyu gwiji ametangaza kuwa baada ya kuachana na Tanasha Donna miezi mitano iliyopita, ameamua kutafuta jiko na kwa sasa ako kwenye uhusiano mpya.

diamond platnumz Hamisa Mobetto
diamond platnumz na Hamisa Mobetto

Diamond Platnumz ambaye ako na mtoto pamoja na tanasha Donna ameelezea ulimwengu kwamba kuna mwanamke anayepanga kufunga naye pingu za maisha. Bingwa huyu ambaye kwa sasa amefikisha miaka thelathini amesema kwa sasa ameamua kutulia na kuanza familia na hana mda na wanawake wengine.

diamond platnumz zari hassan
diamond platnumz na zari hassan

“Sipo single nina mwanamke ninayetaka kuoa. Sisi wengine sasa hivi hatutaki mahusiano, tunataka tuoe. Mwezi wa kumi tarehe mbili nitatimiza miaka 31 na sitaki kuwa tu na mwanamke, sitaki kuwa na kimada , sitaki kuwa na hawara , nataka kuoa,” Diamond aliyasema haya

diamond platnumz wema sepetu
diamond platnumz na wema sepetu

Tunapoongelea kuhusu mahusiano ya kimapenzi, diamond platnumz huzua gumzo hadi watu wengi humkashifu wakidai kuwa haheshimu wanawake. Kumbuka ashawahi kuwa na uhusiano na wema sepetu, zari Hassan ambaye alizaa naye watoto wawili. Pia ako na mtoto mmoja na Hamisa Mobetto

diamond platnumz tanasha Donna
diamond platnumz na tanasha Donna

Wakati alipokuwa na tanasha Donna, wengi walidhania angemuoa. Maneno aliyoyasema Leo kuwa kwa sasa anataka kuoa, aliwahi kuyasema wakati akiwa na tanasha Donna, swali letu ni, mwanamke aliye naye kwa sasa atamuoa ama wembe ni uleule.

Wakati tanasha Donna alipohojiwa, alidai analea mtoto wake bila kusaidiwa na diamond platnumz ambaye ni babake mtoto wake.

Kuna wakati dadake diamond platnumz, Queen Darleen aliwahi kusema diamond hawezi kuoa kwani anaweza poteza mashabiki wake wa kike. Wakati hayuko kwenye uhusiano, wanawake humfurahia na humpa sapoti ikizingatiwa wengine hudhania watakuja kuolewa na yeye.

Soma hii pia (wasanii tajiri Tanzania)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *