HistoriaMaishaMchipuko

Historia ya Amber Ray

Kama wewe ni mtu wa kufuatilia mitandao, basi utakuwa umekutana na mwanadada huyu kwa jina Amber Ray. Ni mwana mitandao na pia mwanamitindo ambaye haogopi chochote kuhusu wanachokisema watu.

Historia ya Amber Ray

Amber Ray ni mwanamke mrembo na anajua kupigania haki yake bila uoga wowote. Kuna wakati ashawahi itwa kahaba Ila hata hakuwafanya chochote waliomuita bali aliwasemehe.

“Siku itakuja mtakuja jutia wenyewe Ila kwa sasa nawasemehe” ndivyo alivyosema amber Ray….”

 

Amber Ray alisema kuwa anampenda Mungu na siku moja ataeleza aliyoyapitia kwenye maisha yake. Bali na kusema anapenda mungu aliongezea na kusema hajaokoka.

amber ray before

Kwa majina kamili amber Ray Anajulikana kama faith makau alizaliwa November tarehe 3 mwaka wa 1992. Kwa sasa ni mwanaharakati wa mitandaoni na jina lake ndilo linalomletea hela.

Kulingana na amber Ray, amefanya Kazi Aina nyingi sana kabla hajafika mahali alipo. Ashawahi uza matumbo, maharagwe na pia alikuwa msaidizi wa wateja ndani ya tovuti ya e-citizen.

Zaheer jihanda and Amber Ray

Aliwahi kuolewa na mwanasiasa kwa jina Zaheer kama mke wa pili. Mke wa kwanza wa Zaheer anayejulikana kama Aaliyah Zaheer aliwahi kumshtumu kwa madai kuwa alitumia uchawi ili aolewe na Zaheer. Kuna wakati amber Ray aliandika kwa Instagram page yake kwamba ameachana na Zaheer.

amber ray latest news

“Nataka kuwapa ujumbe kuhusiana na hatua ninayotaka kuichukua kuhusiana na maisha yangu. Najua hatua hii itawafurahisha wengine wenu kwani wao wanaona kuwa huwa nimewashika mateka…nataka kuwajulisha kwamba nimeachana na Zaheer Merlahi Jihanda na msiwahi nihushisha kabisa na yeye na familia yake kwa jumla…” Aliandika amber Ray

Baada ya kukatisha uhusiano wake na Zaheer, amber Ray Ali date’ wanaume kadhaa huku akiapa kwamba hatawahi kuwa mke wa pili kwa mwanaume yeyote.

Brown mauzo and Amber Ray
Amber Ray na Brown mauzo

Baada ya mda, Faith makau alijitokeza na kusema ameolewa na Jamal “Rohosafi” Marlow kama mke wa pili. Kwenye mahojiano, Jamal alimtetea amber Ray huku akisema amebadilika na kuongeza kwamba anampenda sana. Pia alisema kuwa na uhusiano na amber Ray hakutamfanya Jamal aachane na mke wake wa kwanza.

Amber Ray andJamal Rohosafi
Amber Ray na Jamal

Jamal alikutana na mke wake wa kwanza akiwa shule ya upili. Baadae wawili hawa walioana na wakapata watoto. Jamal alisema anampenda mke wake wa kwanza huku akiongeza kuwa atazidi kuwatuza watoto wake.

Amber Ray ni mama wa mtoto mmoja kwa jina Gavin. Ni mtoto anayevutia na mamake hupenda ku post picha zake kwenye mitandao.

Amber Ray son

Faith makau haijawahi kuongea sana kuhusu wazazi wake hata ni vigumu kuwaweka kwa mitandao. Kuna siku moja tu aliandika kisa cha Babake. Amber Ray anasema Kuna mda Babake alitaka kumfukuza nyumbani kwani alikataa kuolewa na mwanaume mmoja ambaye alikuwa tayari kutoa posa. Hii ndio historia ya Amber Ray Asanteni sana kwa kufuatilia habari zetu hapa mwangaza news.

Soma hii pia : Historia ya bahati

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *