MaishaSanaa

Historia ya Ben Githae ( Tano tena)

Historia ya Ben Githae ( Tano tena); Ben Githae ni mwanamziki kutokea nchi ya kenya. Msanii huyu ako na umri wa miaka 47. Ben Githae Anajulikana kwani yeye alikuwa mmoja wa wale wasanii walimfanyia rais Uhuru kenyatta kampeni mpaka akanyakua kiti Cha urais.

Ben Githae tano tena

Ben Githae Anajulikana sehemu za ukikuyuni kwani nyimbo zake nyingi hutumia lugha ya kikuyu. Amekuwa kwa Sanaa ya mziki kwa miaka mingi na nyimbo zake nyingi zajulikana kenya mzima. Amewahi kushinda tuzo nyingi sana. Mwaka wa 2013, Ben Githae aliachia nyimbo ya “Tano tena” ambayo inaaminika kubadilisha maisha yake kwani ilimlipa donge nono.

Maisha na masomo ya Ben Githae

Alizaliwa sehemu inayojulikana kama Gatundu. Ben Githae alikuwa yuwaimba wakati wenzake walikuwa wakichuna kahawa shambani. Alisomea shule ya msingi ya Muthurumbi. Akiwa huko shuleni, Ben Githae alikuwa yuandikia wenzake nyimbo. Wengi walimbandika jina na kumuita radio ndogo kwani alikuwa yuashika nyimbo yoyote ile baada ya kuiskiza Mara mbili tu.

Ben Githae songs

Ben Githae aliendelea na masomo yake katika shule ya upili ya GIturo boys high school kwenye alihitimu na kupata grade C plus. Nyanyake alimuajiri Kazi kwake kwa kiwanda cha kusaga unga.

Mwaka wa 1994, ben Githae aliokoka na akaanza kuandika kuimba nyimbo za kumsifu mungu. Wakati huo msanii wake wa karibu alikuwa ni Jane muthoni. Wawili Hawa walikuwa marafiki na walikuwa wakiongoza kwaya kanisani mwao.

ben Githae defend himself on tano tena

Ben Githae aliamua kutoendelea na masomo yake ili aendeleze talanta yake ya mziki. Hii ilimkashirisha sana mamake kwani alijua wazi kwamba bila masomo, Ben Githae angeharibu maisha yake ya hapo mbeleni.

Mwaka wa 1996, alikutana na Kamaru na akaachia album yake ya kwanza ” “Mwiri Uyu”. Kamaru alimsimamia ben Githae album hiyo kwani Githae hakuwa na pesa.

Baadae aliachia Album ya pili kwa jina ” Chunga ulimi wako” iliyotayarishwa na peter Kigia. Baada ya mda, Ben Githae aliamua kuachia album ya tatu aliyojitayarishia yeye mwenyewe. Album hii ilipata kuzinduliwa na Radio ya Kameme Fm

Kama wasanii wengi walivyo, ni Jambo la kawaida kwao kupatikana na skedo. Mwanamke kwa jina Rose Wanjiru aliwahi kuhojiwa na jarida la Tuko na kusema kuwa yeye na Ben Githae wamezaa mapacha na ben Githae amekataa kuajibika. Rose Wanjiru alisema walikutana na ben Githae mwaka wa 2011 na kuanza uhusiano wa kimapenzi mwaka wa 2012. Mapenzi yao yalichangia uja uzito mwaka wa 2016. Kuwa mja mzito halikuwa Jambo rahisi kwa Rose Wanjiru kwani alitishiwa hata kabla mtoto hajazaliwa. Ben Githae alipoulizwa kuhusu madai hayo alisema yeye hajawahi kataa kuwa ana mapacha na yeye anawasimamia mahitaji yao yote.

Kwenye mahojiano na Massawe Japani, Ben Githae alikubali kumsaliti mke wake kwa kutembea na mke mwingine. Alisema alishaongea na mke wake na akapata msamaha ila hawezi laumu yeyote kwa alichomfanyia mkewe.

“Siwezisema ni lini nilitoka njee ya ndoa lakini wacha niseme kutoka nilitoka. Mpaka ifike hapo ilikua kwa miaka, mke wangu alijua kitambo na ikaleta issues at family level. Zingine tukatatua na zingine tukaamua kuishi nazo. Siwezisema kulikua na issues kwa familia yangu ndio nikatoka njee. Wacha niseme ilikua tu ni tabia mbaya….”

Nyimbo za Ben Githae

 1. Tabia mbaya
 2. Glory to glory
 3. Uhuruto tano tena
 4. Mere Makire
 5. Irathimo Ciakwa
 6. Kunuthirwo Uru
 7. Maya ni Mabataro
 8. Niundu Wa Wendo
 9. Utalia
 10. Timiza Maono
 11. Tigai Tu
 12. Uroneneha
 13. Mwambararagia
 14. Kioneki
 15. Wee Niwe Ngwenda
 16. Maya Maundu
 17. Watoto Wanna Haki
 18. Ucio Niwe Ngai
 19. Ageria Niekuremwo
 20. Oya Wendo Wakwa
 21. Roho Wa Kaini
 22. Nii Tinie Mwathani
 23. Kiande Ini
 24. Kaba Kwirayia
 25. Ndirwekora
 26. Vita Nyumbani
 27.  Mlianza na Roho
 28. Fanya Kitendo
 29. Guthii ni Guthii
 30. Nimarekwo Mendane

Soma hii ( Waigizaji wa Zora Citizen Tv)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *