HistoriaMaishaMchipukoMzikiSanaa

Historia ya Diamond platnumz

wengi wanaifahamu historia ya Diamond platnumz Ila Kuna vitu vichache ambazo labda hawajapata nafasi ya kuzijua. Kwa majina kamili msanii huyu Anajulikana kama Nasibu Abdul Juma. Ni msanii tuanaweza sema anaongoza afrika mashariki na mziki wake umepenya ulimwengu mzima.

Ametokea nchi ya Tanzania na anafanya mziki aina ya bongo flava. Alijulikana kimataifa kupitia nyimbo yake ya “my number one”. Nyimbo hii ipo aina mbili kwani alifanya moja akiwa peke yake na nyengine akafanya na msanii Davido kutoka nchi ya Nigeria. Colabo hii ilileta manufaa kwa Diamond platnumz kwani alianza kupata kuchezwa kwa vyombo vya habari vya kimataifa.

Historia ya diamond platnumz

Diamond ana miaka ngapi?

Nasibu Abdul Juma anayejulikana kama diamond platnumz alizaliwa tarehe mbili mwezi wa nane mwaka wa 1989 mjini Dar es salaam Tanzania. Alikulia sehemu inayojulikana kama Tandale huku wakiishi na mamake na nyanyake kwa nyumba moja.

Familia ya Diamond platnumz

Mnamo tarehe 6/O8/2015, diamond platnumz alitangaza kupitia Instagram kwamba yeye na zari Hassan walikuwa wanategemea kupata mtoto na baadae alizaliwa na kupewa jina la¬† Lattiffah Ila wengi wanamfahamu kama “Tiffah”

Zari Hassan diamond platnumz Tiffah familia ya Diamond platnumz

 

Baadae walizaa mtoto mwingine wa kiume na zari Hassan ila uhusiano wao ulifika kikomo baada ya diamond platnumz kuwa na uhusiano mwingine na hamisa mobetto. Kwa bahati mbaya ama nzuri, hamisa mobetto alipata uja uzito na kumzalia Diamond mtoto.

Diamond hakukomea hapo kwani alianza uhusiano mpya na tanasha kutoka nchi ya Kenya na wakazaa naye mtoto kwa jina Naseeb junior. Wawili hawa waliachana na mpaka sasa diamond hajaoa mwanamke mwingine Ila anaonekana akitoka na wanawake tofauti kutoka nchi za ulaya.

Tuzo alizoahiriki diamond platnumz.

Mnamo may 3 mwaka wa 2014, Diamond platnumz alivunja rekodi baada ya kushinda tuzo saba katiza tuzo za Tanzania music awards zikiwemo best male writer, best male artist, best song writer na pia best male entertainer of the year.

Safari ya mziki ya Diamond platnumz

Diamond platnumz alianza kupenda mziki akiwa shule. Akiwa darasa la nne, Diamond alikuwa akiigiza wasanii wa Tanzania na wale wa kimataifa. Kuna wakati kwa tamasha alikuwa akitumbuiza watu kwa kuimba nyimbo za wasanii mbalimbali. Mamake Diamond almaarufu kama mama dangote alikuwa mstari wa mbele kusapoti kipaji Cha Diamond platnumz kwani hata alikuwa akimnunulia diamond albums za wasanii ili aweze kufuatilia nyimbo zao kwa kuyashika maneno yote ya hizo nyimbo.

Akialikwa kwa sherehe, mama dangote alikuwa akimpeleka na zaidi alikuwa akimtafutia tamasha za kusaka vipaji akijua siku moja mwanawe atapata mtu wa kusapoti kipaji chake.

Kwa sasa Diamond Platnumz Anajulikana ulimwengu mzima na ameachia zaidi ya nyimbo mia mbili.

Utajiri wa Diamond

diamond platnumz ana miaka mingapi

Diamond Platnumz ndiye msanii anayesemekana kulipwa hela nyingi katika afrika mashariki. Pia ameorodheshwa bara nzima la afrika kama mmoja wa wasanii tajiri. Mziki wake umeuza sana katika mitandao ( music downloads. Amepiga music tour nyingi sana ulimwengu mzima na kampuni nyingi humtumia kwa matangazo ya biashara ikiwemo coca-cola ambayo ni kampuni kubwa duniani.

Kumbuka Diamond Platnumz ndiye mwanzilishi wa WCB ( wasafi ) label ambapo amekuza wasanii wengi akiwemo harmonize, Rayvanny, Mbosso, Lavalava na Zuchu. Wasafi label inamuingizia mamilioni ya pesa bila kusahau wasafi Tv na Wasafi F.m.

Soma hii pia : maisha ya harmonize

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *