International

Historia ya Ferdinand Omanyala Omurwan

Mashindano ya the Tokyo Olympics yamefungua njia kwa mkenya Ferdinand Omanyala Omurwa. Hii ni kwa sababu mkenya huyu anaipeperusha bendera ya Kenya kwa ushindi mkubwa.

ferdinand omanyala family

Ferdinand Omanyala Omurwa ni mzaliwa wa county ya bungoma nchini kenya. Alizaliwa mwaka wa 1996 na alifikisha miaka 25 mnamo august 3  mwaka wa 2021. Wazazi wake wamekuwa wakimpa sapoti michezoni akiwa bado mtoto. Amezaliwa katika familia ya ndugu watano

Masomo ya Omanyala

Alisomea county ya bungoma kabla ya kujiunga na chuo kikuu Cha university of Nairobi kwa masomo zaidi. Alianza kushiriki kwenye mchezo wa rugby akiwa shule ya upili ya kamusinga high school na hapo ndipo safari yake ya mchezo wa rugby ilipoanzia. Kwa sasa Omanyala anaendelea masomo yake zaidi katika chuo kikuu Cha Nairobi.

Ferdinand Omanyala Omurwa alianza kuvutiwa katika michezo akiwa bado mtoto. Akiwa chuo kikuu Cha Nairobi aliendelea na kucheza mchezo wa rugby na hapo baadae ndio akaingia kwa riadha. Kwa sasa anakimbia mbio za mita mia moja na anafanya vizuri.

Ferdinand Omanyala background

Katika mashindano yaliyoko Tokyo 2020 ambayo yalihairishwa kwa sababu ya janga la covid ferdinand omanyala alifanya maajabu. Kwenye mashindano hayo, Omanyala aliibuka mshindi katika semifinals za 100m na kuweka rekodi ya dunia ya sekude kumi.

Ushindi wake umepokelewa kwa furaha na familia yake huko bungoma na nchi nzima kwa jumla. Ameahidi kufanya bidii na kupeperusha bendera juu zaidi

Ferdinand Omanyala wife tribe

Mamake Ferdinand Omanyala amekuwa akimpa sapoti tokea akiwa mdogo. Kushinda juzi huko Tokyo kulimfurahisha mamake sana na akaamua kumletea chakula uwanja wa ndege punde tu atakapowasili.

Omanyala anapenda samaki na ugali. Ameoa mwanamke mrembo kwa jina Laventa Omanyala. Wawili hawa Wana mtoto mmoja kwa jina Quinton Finn. Kwenye mahojiano, Omanyala alisema kwamba mke wake alikuwa akimlipia Kodi ya nyumba wakati yeye hakuwa na kazi. Ferdinand Omanyala Omurwa aliahidi mke wake kwamba kwa sasa atamsimamia kila kitu kwani hapo mwanzoni mke wake alimsaidia sana.

ferdinand omanyala wife

Kwa sasa tunakomea hapo kuhusu Historia ya Ferdinand Omanyala Omurwa. Kwa mengi zaidi zidi kufuatilia tovuti yetu ya mwangaza news.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *