HistoriaMaisha

Historia ya Hamisa Mobetto

Hamisa Mobetto ni mmoja wa wanawake warembo nchini Tanzania. Hutumiwa sana na wasanii kwa video zao kama video vixen. Ni mwanamitindo, mwanamziki na pia mfanyi biashara. Kampuni kadhaa zimemtumia katika matangazo ya biashara. Pia anamiliki kampuni yake mwenyewe kwa jina Mobetto styles.

Wakati tunapo wahesabu wanawake ambao wamewahi kutoka kimapenzi na diamond Platnumz, hatuwezi kosa kumtaja hamisa mobetto. Wawili hawa waliwahi kuwa wapenzi na wakazaa pamoja.

Hamisa Mobetto alizaliwa mwaka wa 1994, tarehe 10 mwezi wa December maeneo ya mwanza nchini Tanzania. kwa sasa tunaweza sema ako na miaka 27 mwaka wa 2021. Kila tarehe kumi December, hamisa mobetto huandaa sherehe ya kukata na shoka, kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Masomo ya hamisa Mobetto

Hamisa Mobetto alisomea shule ya msingi ya Mabatini na kuendelea na masomo ya shule ya upili katika shule ya St. Kayumba secondary school.

Maisha yake kama mwanamitindo

Hamisa Mobetto ni mwanamitindo anayeheshimika sana. Anapendwa sana na umbo lake lavutia wengi. Ni hivi majuzi ilisemekana kwamba mrembo huyu anatoka na Rick Ross. Ako na wafuasi wengi sana katika kurasa zake ndani ya mitandao.

Kutokana na hawa wafuasi, hamisa Mobetto hutumiwa na kampuni nyingi kuwafanyia matangazo kwani kampuni zenyewe zinafahamu kuwa akifanya matangazo itawafikia wengi

Hamisa Mobetto ashatumiwa na diamond kwa video ya “Salome” iliyogonga vichwa vya habari. Ni wakati huohuo ambapo wawili hawa walikuwa kwa uhusiano wa Siri uliochangia kuachana kwa diamond platnumz na zari Hassan. Alikiba pia ashawahi mtumia hamisa Mobetto kwa video ya nyimbo yake ‘Dodo’

Nyimbo zake hamisa Mobetto ni kama vile; Sensema, Madam Hero, My love na sawa. Japo Diamond platnumz na hamisa Wana mtoto pamoja, Diamond hajawahi tangaza kuwa wawili hawa ni wapenzi. Kumbuka mamake diamond hampendi kabisa hamisa Mobetto hata hajawahi ku post mtoto wa hamisa kwa kurasa zake za instagram na Facebook.

Watoto wa hamisa  Mobetto

Mrembo huyu amebarikiwa na watoto wawili. Msichana pamoja na mvulana. Mtoto wa kwanza Anajulikana kama Fantasy mwenye umri wa miaka sita na Deedaylan Abdul Naseeb ambaye ana miaka mitatu. Fantasy ni mtoto wa dj maarufu kutoka tanzania kwa jina Dj Majizzo naye Daylan mtoto wake Diamond platnumz a.k.a Naseeb chini Dangote

Baada ya kuachia nyimbo yake ya Jeje, diamond platnumz aliwahi ku post Hamisa Mobetto akicheza nyimbo ya “Jeje”. Wengi walijiuliza maswali mengi bila kupata majibu na kudhania labda wawili hawa walikuwa wanaendeleza uhusiano wao. Baada ya tetesi hilo, Hamisa Mobetto aliwajibu na kusema yeye na Diamond platnumz hakuna hata siku moja watakuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi tena.

Mtoto wa diamond na hamisa Mobetto

mtoto wa hamisa Mobetto

Kama nilivyosema hapo awali, mmoja wa Watoto hao wawili anajulikana kama Deedaylan Abdul Naseeb. Alizaliwa tarehe 7 august, 2017. Mwanzo kabisa Diamond Platnumz alimkana mwanawe na ikabidi vipimo vya DNA viweze kufanyika. Baada ya majibu kuonyesha wazi kwamba mtoto yule ni wa diamond platnumz, chibu a.k.a diamond alimkubali.

Wakati Deedaylan anazaliwa, Diamond alikuwa kwenye uhusiano na zari Hassan kutoka nchi ya Uganda. Hii ndio sababu iliyowafanya wawili hawa kuachana. Baadae Diamond platnumz alipatana na tanasha Donna Oketch kutoka Kenya na wakazaa naye mtoto

Mpenzi wa hamisa Mobetto

Hamisa amekuwa na mchumba kutoka emerika kwa jina Joshua ( Josh) Adeyeye. Wawili hao walikutana wakati hamisa Mobetto alikuwa amesafiri marekani kwa shughuli za biashara. Josh ana miaka 28 na alikuwa mchezaji wa basketball pia ni mwanamitindo. Hamisa Mobetto aliwahi kumtumia josh kwa video ya nyimbo yake ” Tunaendana” kwa sasa inasemekana wawili hawa waliachana.

Gari ya hamisa  Mobetto

gari la hamisa Mobetto

Hamisa Mobetto aligonga vichwa vya habari baada ya kununua gari aina ya Land Rover discovery kwa pesa yake mwenyewe. Alitangaza kumiliki gari wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa mwaka wa 2020. Pia aliweza ku post video ya gari hiyo kwa page yake ya Instagram n kuzua maswali mengi wengi wakisema gari hilo sio lake Ila anatafuta “Kiki” .

” Asante Mungu kwa kunioa zaidi ya chenye nahitaji ilikuwa ni sherehe kwa mpigo kwani tumesherehekea kuzaliwa kwangu na kwa mamangu pia. Nashukuru familia yangu na marafiki kwa kujumuika nami.. Asanteni na baraka tele kwa miaka ilioko mbele yetu… Ndivyo alivyoandika hamisa Mobetto kwa Instagram page yake.”

Nyumba ya hamisa Mobetto

nyumba ya hamisa Mobetto

Hamisa Mobetto alishangaza wengi sana baada ya kuonyesha nyumba yake inayosemekana kumgharimu milioni 600 za Tanzania. Hii ni baada ya wengi kusema yeye ni maskini baada ya Diamond platnumz kumkataa. Kulingana na hamisa, yeye anajitegemea na nyumba yake alinunua na pesa zake mwenyewe.

Utajiri wa hamisa Mobetto

Utajiri wa hamisa Mobetto kwa sasa unakisiwa kuwa $3 million. Hupata pesa kupitia kampuni yake, matangazo ya biashara kutumika kama video vixen na pia ni mfanyi biashara.

Wazazi wa hamisa Mobetto

Alilelewa na baba wa kambo. Kulingana na yeye, Babake wa kambo alikuwa mtu mzuri, mpole na alimpenda sana. Hamisa Mobetto hakumdharau Babake wa kambo hata kama hakuwa Babake halisi. Ukarimu wa Babake hamisa ulimfanya kutangaza kuwa mwanaume atakayemuoa lazima awe kama Babake wa kambo.

Mara ya kwanza kwa hamisa kukutana na Babake mzazi ilikuwa mwaka wa 2007, wakati huu hamisa walikuwa wameenda kununua bidhaa za sikuku ya Christmas. Hapo ndipo aliposikia mtu akiitana “Mum’ kugeuka akakutana macho kwa macho na Babake mzazi. Hakufurahia sana kwani alitaka Mara ya kwanza wakikutana iwe ni sherehe ya kimataifa.

Hakuwa na la kufanya Ila kupiga goti na kumsalimia Babake kama alipoagizwa. Hapo ndipo akagundua kwamba alikuwa anafana kabisa naye. Walijaribu kurudisha uhusiano kama baba na mtoto lakini kwa bahati mbaya Babake mzazi aliaga dunia miaka miwili baadae.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *