MaishaMchipukoSanaa

Historia ya Harmonize : Maisha ya harmonize

Kuna wengi wanamfahamu msanii huyu Ila hawajui vizuri historia ya harmonize. Kwa majina kamili Anajulikana kama Rajabu Abdul kahali. Ni msanii kutokea nchi ya Tanzania na anafanya mziki wa aina ya bongo flava. Wengi wanamfahamu kama harmonize, jina lake la kisanii.

Jina yake ya Rajabu hupewa watoto wavulana waliozaliwa mwezi wa saba Kulingana na calendar ya kiisilamu japo kiukweli harmonize hakuzaliwa huo mwezi

Abdul humanisha mtumwa kwa kiarabu na pia inamanisha dhoruba Kali. Kwa kweli harmonize ni dhoruba Kali nchini Tanzania kimziki kwani mziki wake upo juu sana. Katika historia ya Harmonize nadhani pia umejifunza maana ya majina yake.

Kabla ya mkataba wake na Diamond Platnumz mmiliki wa wasafi media WCB, harmonize alikuwa mtoto wa mtaani aliyekuwa amechoka na kuishi.

Kujulikana kwake ni wakati alipochukuliwa na diamond kwenye record label yake. Alirekodi nyimbo nyingi kwenye label ya wasafi hadi baadae alipotoka wasafi na kufungua label yake mpya kwa jina Konde music worldwide. Kwenye label yake ndipo amerekodi album yake ya kwanza kwa jina “Afro East”

Wakati akiwa label ya wasafi, harmonize aliachia Ep ( extended play ) kwa jina ” Afro Bongo” iliyohushisha wasanii wengi wakiwemo wasanii kutoka nchi mbalimbali barani afrika.

Kwa sasa inasemekana anafanya project mpya Ila bado haijajulikana ni project aina gani.

Utajiri wa harmonize

Tunapoongelea kuhusu historia ya harmonize basi lazima tutagusia label ya WCB. Harmonize alianza kuingiza hela ndefu wakati alijiunga na wasafi. Baada ya kutoka wasafi record, harmonize alisemekana kupoteza hela nyingi sana kwani alihitajika kulipa kabla ya kuondoka label hiyo kwa kuvunja mkataba.

Hata baada ya kulipa hela nyingi, harmonize bado yupo vizuri kihela kwani label ya konde music worldwide inamuingizia mamilioni. Bado kabisa haijajulikana pesa zenye anapata kwa sasa Ila ni pesa nyingi na huenda ikawa baada ya Diamond Platnumz, harmonize atakuwa msanii wa pili mwenye pesa nyingi.

Umri wa harmonize

Harmonize alizaliwa March 1990 hii Ina maana mwaka wa 2021 ako na miaka 31.

Watoto wa Harmonize

Kama mwaka mmoja uliyopita, harmonize alitangaza kuwa atakuwa na mtoto na Sarah Michelloti. Baadae ilisemekana kwamba mimba ilitoka. Kuna wakati alionekana na mtoto kwenye mitandao aliyedai ni mtoto wake Ila bado haijafahamika kama ni kweli.

Mpenzi wa harmonize

Harmonize alikuwa na mpenzi kutoka Italy kwa jina Sarah Michelloti. Wawili hawa wamekuwa pamoja Ila inasemekana kwa sasa wameachana. Ni hivi majuzi alianza uhusiano na kajala Ila pia wakaachana kwa kile kikisomekana kwamba alikuwa pia na uhusiano wa kimapenzi na mtoto wa kajala anayejulikana kama Paula kajala.

Nyumba ya harmonize na magari

maisha ya harmonize gari ya Harmonize

Mziki wake unalipa vizuri na hii imemuezesha harmonize kumiliki magari makubwa na nyumba ya kifahari. Kuna mda kupitia Instagram page yake ali post nyumba yake ya kifahari iliyoko Katikati ya jiji la dar es salaam.

Harmonize kwenye label yake ana mkataba na wasanii kama vile country boy, ibraah na Angela. Wasanii hawa wanafanya vizuri kimziki kwani wamepokelewa vizuri nchini tanzania na nchi jirani. Ni hayo tu kwa Leo kuhusiana na historia ya harmonize.

Soma hii pia : historia ya alikiba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *