Historia

Historia Ya Jay Melody

Baada ya kuachia sugar, Jay melody alianza kujulikana na Kugonga vichwa vya habari ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania. Historia ya Jay melody ni ya kipekee kwani ametoka kwenye familia ambayo haina uwezo ila kwa sasa anategemewa na familia yake. Karibu mwangaza news uweze kumfahamu zaidi Jay Melody.

Majina kamili ya Jay Melody na mwaka wa Kuzaliwa

Majina kamili ya Jay Melody anajulikana kama Sharif Said Juma. Gwiji huyu alizaliwa mnamo tarehe 12 mwezi wa sita (June) mwaka wa 1997. Jay melody ni jina yake ya kimziki ila wengi wanamfahamu na jina hilo.

Jay melody ni mwandishi mkali sana na kama umesikiza nyimbo zake kama vile sugar na Ile ya Nakupenda utaelewa zaidi uwezo wa msanii huyu kutoka Tanzania.

Tukirudi kwenye maisha yake ya utotoni, Jay Melody alizaliwa ndani ya hosipitali ya Mwananyamala iliyoko dar es salaam, Tanzania wazazi wake wakiwa bwana na bibi said juma

Picha za Jay Melody

Masomo ya jay Melody

Kati ya mwaka wa 2005 na 2011, Jay melody alikuwa shule ya msingi ya Muhalitani iliyoko Tandale, vitongoji duni mjini dar es salaam. Alimaliza masomo yake ya shule ya msingi mwaka wa 2011.

Mwaka wa 2012, Jay melody alijiunga na shule ya upili ya Bunju na kumaliza mwaka wa 2015 na inasemekana aliweza kupita vizuri baada ya kupata alama za Juu zaidi kwenye mtihani wa kimataifa.

Mwaka wa 2016 ndio ulikuwa mwaka wa Jay Melody kujiunga na Wana mziki wenzake baada ya kupokelewa ndani ya Tanzania house of talent ( THT) ili ajifunze mengi inayohusiana na mziki

Baada ya mwaka mmoja Jay Melody alichukuliwa na record label ya Genius Ruger Mutahaba ambayo ni Kati ya Lebo kubwa nchini Tanzania. Kwenye label hiyo alijifunza mengi na alikuwa tayari kuachia kazi

Jay Melody aliachia album yake ya kwanza kwa jina Garoka. Kama unafahamu nyimbo ya Nandy kwa jina Kivuruge, basi jua kuwa aliyeiandika nyimbo hii sio mwingine ila jay Melody.

Mpenzi wa Jay melody

Mpenzi wa Jay melody

Kwa sasa Jay Melody anadai kuwa bado Yuko single na anafurahia maisha kwanza ila anasema hayuko tayari kuoa hivi karibuni kwani kwa sasa ana mambo mengi kuhisiana na mziki wake na hana mda na wanawake

Utajiri wa Jay Melody

Kwa sasa Jay Melody anasemekana kuingiza hela ndefu kwani nyimbo yake ya nakupenda pamoja na sugar zimefanya ajukikane zaidi.

Hiyo ndio historia ya Jay Melody na Kwa sasa waweza tazama Nakupenda yake Jay Melody ili uweze kupata burudani hapa mwangaza kwa kubonyeza link ifuatayo.

Pia soma, Historia ya Marioo na utajiri wake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *