HistoriaMaisha

Historia ya Jovial

Jovial ni msanii maarufu kutoka nchini Kenya. Kwa sasa anaishi Nairobi japo kuwa alizaliwa Mombasa. Alianza safari yake ya mziki akiwa mkoani pwani. Iliwahi semekana kwamba ako na uhusiano na Otile brown baada ya kufanya kazi naye ambapo nyingi za kazi hizo zilikuwa za mapenzi. Zidi kutegea hapa mwangaza news ili tuweze kukujuza mengi kuhusiana na historia ya jovial.

Akiwa shule ya Msingi, Jovial alikuwa ni mtu wa furaha mda wowote ule. Alikuwa sio mtu wa kukasirika na hapo ndipo alipojipatia jina la Jovial kumanisha ni mtu mwenye furaha. Jina hili alipewa na mwalimu wake aliyekuwa mkaribu wake.

Jovial na Willy Paul.

Jovial and willy paul

Willy paul amekuwa akidai anamtaka Jovial huku akiapa kuwa Jovial akija kwake atapata Mapenzi yenye hajawahi pata kwa mwanamume mwingine yote. Juzi alimpokea airport baada ya safari ya jovial kutoka Mombasa

Umri wa jovial

Jovial alizaliwa tarehe moja January mwaka wa 1992. Majina yake kamili anajulikana kama Juliet Mariam Ayub. Alizaliwa mjini Mombasa sehemu inayojulikana kama Kisauni. Jovial ana uwezo wa kuandika nyimbo, kuimba na pia performance yake iko juu sana.

Jovial Age

Safari ya mziki wa msanii Jovial

Kama wasanii wengine wale, jovial alianza kupenda mziki akiwa mdogo. Mamake alikuwa shabiki wake mkubwa sana na mpaka wa Leo anamshukuru kwani amechangia pakubwa sana kwenye safari yake ya mziki.

Akiwa shuleni, jovial alikuwa mwanakwaya.  Alipata umaarufu kwani alikuwa na sauti yenye uwezo mkubwa sana. Kuzaliwa mkoa wa pwani kumechangia pakubwa sana katika mziki wake kwani ana uwezo mkubwa sana wa kuandika na kuimba nyimbo kwa lugha ya kiswahili.

Jovial hufanya mziki aina ya R&B, Afro fusion pamoja na Zuok twist. Kabla ya kuhamia Nairobi, jovial alikuwa akirekodi na producer Amz ambaye anajulikana sana mkoani pwani.

Kuna mda jovial alitaka kuacha mziki baada ya kuamua kwenda kufanya kazi za ndani saudia. Akiwa katika pilkapilka za kupanga safari yake, Jovial alikutana na David Guoro ambaye ndiye meneja wake kwa sasa. David Guoro alipendezwa sana na talanta ya Jovial na baada ya kusikia masaibu aliyokuwa akipitia Jovial, David aliamua kumsimamia kazi zake za mziki.

Jovial photos

Nyimbo ya kwanza ya Jovial ambayo iliweza kufanya ajulikane zaidi ilikuwa yajulikana kama chanda chema ambayo ilitayarishwa na producer Amz. Nyimbo hii iliweza kupata umaarufu kwani ilipata nafasi kwenye radio za hapa nchini Kenya na Tanzania kwa jumla. Pia iliweza kumsaidia jovial kuongeza wafuasi wengi kwani kila mtu alitaka kumfahamu msanii huyu mwenye sauti nzuri.

Kufikia sasa Jovial amefanya kolabo na wasanii kadhaa wa E. Africa wakiwemo Darasa na Marioo kutoka Tanzania, Otile brown, Arrow bwoy, Mejja na wengine wengi. Pakua ambayo ni colabo yake na Mejja iko na zaidi ya 3 millions views kwenye YouTube. Kulingana na Jovial, kufaulu kwake kimziki kumesababishwa na bidii yake na timu nzima inayomuongoza bila kumusahau Mwenyezi Mungu ambaye amempa sauti nzuri na talanta ya hali ya juu.

Jovial na Otile brown

Jovial Otile brown

Jovial na Otile wamekuwa wakifanya kazi pamoja mpaka wengi wakadhania wawili hawa wako kwenye uhusiano. Kati ya nyimbo walizofanya pamoja ni; Jeraha. Kuna mda ilisemekana kwamba Otile brown amemununulia Jovial gari ila maajabu ni kwamba mpaka Leo hakuna ashawahi ona hiyo gari.

Baada ya kufanya kazi kwa mda, kulitokea utofauti kati ya wawili hawa na kila mtu akaenda kivyake. Mpaka Leo haijajulikana ni kitu gani kilichangia wawili hawa kuachana. Nyimbo zingine walizofanya pamoja ni zichune, Such kinda love na Amor. Nyimbo hizi zote zipo na zaidi ya views million mbili kwenye YouTube channel ya Otile brown

Mpenzi wa Jovial

Japo ana mtoto, bado hajaeka wazi babake mzazi ni nani. Kulingana na habari za hapa na pale, Jovial waliachana na baba mtoto na Kwa sasa hajulikani kama ako kwa uhusiano mwingine au la.

Utajiri wa Jovial

Bali ya uigizaji, jovial pia ni muigizaji. Aliwahi igiza kwa tamthilia ya Kovu ndani ya maisha magic. Uigizaji una hela nyingi tena ya kueleweka hiyo inamanisha jovial ana utajiri mkubwa maana anapata pesa kupitia mziki na uigizaji. Kwa sasa hatuwezi sema utajiri kamili wa jovial ila tunaweza sema jovial anafurahia maisha kama wasanii wengine wakubwa.

Nyimbo za Jovial

Jovial songs

Kama nikivyotangulia kusema, Jovial amefanya kolabo na wasanii kadhaa wa afrika mashariki na pia ana nyimbo zake pia ambazo ameachia. Baadhi ya nyimbo za jovial ni kama zifuatazo

  1. Jeraha featuring Otile Brown
  2. Pakua Ft. Mejja
  3. Zichune Ft. Otile Brown
  4. Unanikosha
  5. Usiku Mmoja featuring Darassa
  6. Chechemea
  7. Kioo Featuring Arrow Bwoy

 

Hiyo ndio Historia ya Jovial, tutakomea hapo Kwa sasa ila tutazidi wajulisha mengi kuhusiana na Jovial na wasanii wengine barani afrika. Zidi kutegea mwangaza news kwa habari zaidi

Soma pia, Historia ya Marioo hapa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *