Historia

Historia ya Kajala Masanja, umri na uhusiano na Harmonize

Kajala Masanja amegonga vichwa vya habari kwa mda sasa baada ya kuregeleana na Harmonize. Kumbuka wawili hawa walikuwa wamekosana na Kajala Masanja alikuwa hataki kumuona Harmonize karibu na yeye. Historia ya Kajala Masanja ni ya kuigwa na wengi kwani hata kama amepitia mengi kwenye mahusiano yake, bado anaokena kutokata tamaa katika swala nzima la mapenzi.

Umri wa Kajala Masanja

Kajala photos

Kajala alizaliwa tarehe 22July mwaka wa 1983, hii Ina maana mwaka wa 2022, Kajala ako na miaka 39.

Safari ya uigizaji

Kwa wale wanaofuatilia sinema za Tanzania ama Bongo movies, watakuwa wanamfahamu sana gwiji huyu. Kajala alianza kuigiza mda mrefu uliopita akiwa pamoja na wema sepetu. Mwaka wa 2016, Kajala aliweza kushinda tuzo la east Africa television awards kwa kitengo Cha best Tv personality.

Movie za Kajala Masanja

Kati ya sinema zenye Kajala Masanja aliwahi kuigiza ni kama vile “Kijiji Cha tambua haki” akiwa ameshilikiana na¬† Steven Kanumba ambaye kwa sasa ni marehemu. Sinema hii ilifanyika mwaka wa 2012. Kabla ya sinema hii, Kajala pia aliweza kuhusika katika sinema iitwayo “Basilisa” mwaka wa 2011. Sinema nyengine aliyoigiza Kajala ni “Jeraha la Moyo” na zinginezo.

Mume wa Kajala Masanja wa kwanza

Kajala alikuwa na uhusiano na p frank majani, mtayarishaji wa mziki. Wawili hawa walipata mtoto wa kike kwa jina Paula ambaye kwa sasa ako kwenye uhusiano na Rayvanny msanii aliyekuwa wasafi ila kwa sasa ametoka wasafi.

Harmonize na Kajala Masanja

Kajala na harmonize

Baadaye, Kajala alianza uhusiano na Harmonize ila walikosana. Hivi majuzi wawili hawa walipatana na kwa sasa wapo pamoja tena.

Paula ambaye ni mwanaye Kajala alionekana kupinga mahusiano ya wawili hawa ila kwa sasa inaonekana amekubali mamake awe na Harmonize.

Utajiri wa Kajala Masanja

Kajala Masanja Instagram

Filamu ni sekta inayofanya vizuri sanasana nchini Tanzania. Kajala amekuwa kwa filamu kwa mda sasa na ni kati ya wale waliofanikiwa sana. Kajala Masanja anesemeka kuwa na utajiri wa zaidi ya $300,000.

Soma pia Historia ya Paula Kajala

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *