HistoriaSports

Historia ya Lionel Messi

Sio watu Wengi wanaifahamu vizuri historia ya Lionel Messi. Ningependa kuichukua nafasi hii nikufahamishe mengi zaidi kuhusiana na historia yake kupitia tovuti yetu ya mwangaza news.

Lionel Messi ni mchezaji wa timu ya PSG japo kwa mda mrefu sana amechezea FC Barcelona na timu ya Argentina kama timu yake ya taifa. Ni Kati ya wachezaji waliofunga magoli nyingi sana katika maisha yake akiwa mchezaji wa mpira wa miguu. Lionel Messi pia ameshinda tuzo nyingi sana na anajulikana dunia nzima.

Akiwa na umri wa miaka kumi na tatu, Messi alihama kutoka Argentina mpaka Spain baada ya FC Barcelona kukubali kumsimamia matibabu yake

Picha za Lionel Messi utotoni

Hapo ndipo alijulikana zaidi na kuwa mchezaji bora katika historia ya mpira wa soka. Lionel Messi alisaidia timu yake kushinda tuzo nyingi sana katika ligi tofauti. Mwaka wa 2012, Lionel Messi alishinda kama mchezaji aliyefunga magoli zaidi duniani. Mwaka wa 2019, alipewa jina ya Europe’s ballon d’ ama mshindi wa Mara sita

Lionel Messi alizaliwa June 24 mwaka wa 1987, Rosario nchi ya Argentina. Akiwa mdogo Messi alipenda kuwa karibu na ndugu zake wawili ambo ni wakubwa wake waliopenda kucheza mpira. Akiwa na miaka minane, Messi alichaguliwa kujiunga na Youth system of Newell’s old boys. Hii ni klabu iliyoko maeneo ya Rosario

picha za Lionel Messi

Katika timu hiyo, Lionel Messi ndiye aliyekuwa mchezaji mdogo mwenye kimo kidogo kuliko watoto wengine. Akiwa Youth system of Newell’s old boys, Messi alipatikana na matatizo ya hormone deficiency, tatizo lilokuwa likimfanya Messi asikue. Wazazi wake Jorge na Cecilia waliamua mtoto wao adungwe sindano ya regimen of night growth hormone japo ilikuwa vigumu kwao kusimamia matibabu ya kila mwezi iliyokuwa juu sana.

Akiwa na umri wa miaka 13, Messi alipata nafasi ya kujiunga na Fc Barcelona’s youth academy. Klabu hiyo ikajitolea kusimamia matibabu yake. Hii ilifanya familia ya Messi kuhamia Atlantic na kuanza kuishi Spain.

Mchezaji mwenye magoli mengi duniani 2021

Wengi humfananisha Messi na aliyekuwa mchezaji wa Argentina Diego maradona kwani wote wawili ni wafupi na kimo Chao ni futi tano nchi saba. Lionel Messi amekuwa akichezea timu mbili tu Barcelona na timu ya taifa ya Argentina. Ni hivi majuzi tu alipojiunga na PSG. Messi Alisajiliwa na Barcelona akiwa na umri wa miaka 13.

Mara ya kwanza kuchezea timu ya FC Barcelona, Lionel Messi alikuwa na umri wa miaka kumi na sita. Hii ilimfanya aingie kwa vitabu vya kumbukumbu kama mchezaji mwenye umri mdogo katika historia ya mchezo wa soka. Mwaka wa 2005, aliiwezesha nchi yake ya Argentina kushinda world cup ya wachezaji wasio zidi umri wa miaka 20 huku akifunga magoli mawili kupitia njia ya penalty.

Mwaka wa 2009, Messi na timu yake ya Barcelona walishinda ligi tatu zikiwemo The champions league, la Liga pamoja na Spanish super cup titles. Kumbuka mwako huo pia alishinda FIFA world player of the year honor/Ballon d’Or award.

Historia ya Lionel Messi

Maradona aliyekuwa maarufu wakati huo alimsifia sana Lionel Messi

” Namuona Lionel Messi anacheza tu kama Mimi na tunaendana vitu vingi… Namuona kama mwalimu na mafunzo yake kwenye soka itawasaidia wengi kwani anachokifanya ni tofauti na wachezaji wengine duniani…”

Messi aliweka rekodi nyingi sana na kila siku alizidi kuwa mkali zaidi. Mwaka wa 2010 timu yake fc Barcelona ilishinda tena La Liga pamoja na Spanish super cup championships.

2012, aliweka rekodi nyengine ya kufunga magoli tano kwa mechi moJa ya champions league na baadae akaivunja rekodi ya surpassed Cesar ya magoli 232 ambapo mpaka Leo Lionel Messi ndiye anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi Barcelona.

Mnamo June 30, Mwaka wa 2017, Messi alioa Antonella Roccuzzo aliyekuwa mchumba wake wa miaka mingi na rafiki wa mchezaji mwenzake Lucas scaglia. Messi na Roccuzzo Wana watoto watatu; Thiago aliyezaliwa November 2012, Mateo, aliyezaliwa September 2015 na Ciro mzaliwa March 2018.

familia ya Messi

Messi na Roccuzzo walijuana na Messi akiwa na miaka tano mjini kwao Rosario. Harusi yao ilikuwa kubwa sana na ilipewa jina na gazeti la clarín newspaper kama ” wedding of the century”. Sherehe ya harusi yao ilifanyika katika hoteli ya kifahari huko Rosario. Wanasoka maarufu duniani walikuwemo bila kusahau Shakira ambaye ni mwanamziki mkubwa duniani kutoka nchi ya Colombia.

Hiyo ndio historia ya Lionel Messi na bilashaka ameyafahamu mengi kuhusiana na mchezaji huyu Gwiji. Kumbuka hapa mwangaza news tunaangazia historia za watu wengi maarufu duniani na kwa historia zaidi bonyeza hapa ( Historia) ili uweze kufahamu mengi

Soma hii pia : historia ya Cristiano Ronaldo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *