Historia

Historia ya Marioo : Utajiri wa Marioo

Kwa wale walikuwa wanaulizia kuhusiana na Historia ya Marioo, Leo nitawaeleza mengi kuhusiana msanii huyu gwiji kutoka Tanzania.

Marioo ni msanii ambaye kwa sasa anajulikana zaidi afrika mashariki. Pia ni msanii mwenye amefanya colabo nyingi na wasanii wakubwa afrika nzima kwa jumla. Aliwahi kufanya kazi na sho Madjozi wa afrika kusini inayojulikana kama mama Amina. Pia aliwahi kufanya colabo na Jovial, msanii wa kike nchini Kenya anayefanya vizuri sana kwa sasa. Hii ni historia fupi ya Marioo kutoka nchini Tanzania anayefanya mziki aina ya bongo flava.

Majina kamili ya Marioo na miaka yake

picha za Marioo

Majina kamili, Marioo anajulikana kama Omari Mwanga. Kwa sasa ambapo tupo mwaka wa 2022, msanii huyu ana miaka 27 kwani alizaliwa mwaka wa 1995 Bali na kuimba, Marioo anajua kuandika nyimbo na ashaandikia wasanii wengi wakubwa nyimbo zao. Pia ana uwezo wa kucheza guitar. Marioo hajakuwa kwa usanii kwa miaka mingi ila kwa sasa ako kiwango Cha alikiba na diamond platinumz.

Masomo ya Marioo na maisha yake

Marioo alizaliwa maeneo yanayojulikana kama kibiti nchini Tanzania. Amesoma shule ya msingi ila inasemekana hakuweza kuendelea na masomo ya shule ya upili kwa ukosefu wa karo. Mjombake aliamua kumpeleka gereji ili ajifunze kazi ya kutengeneza magari angalau apate mkate wake wa kila siku.

Wakati akifanya kazi kwenye gereji, mteja wake mmoja aliamua kumsimamia kurekodi kwani aligundua kuwa alikuwa na kipaji Cha uimbaji. Ilikuwa vigumu kwake kuweza kuendelea kimziki kwani hakuwa na hela ya kuezesha mziki wake uweze kuenea sehemu tofauti. Marioo hakufa moyo na mwaka wa 2017, alirekodi nyimbo yake kwa jina ” Dar Kugumu”. Nyimbo hii iliachiliwa mwanzoni wa mwaka wa 2018 ikiwa chini ya instinct Records. Kwa bahati nzuri, nyimbo hii ilipata umaarufu zaidi Tanzania nzima na watu wakamujua na kumuelewa Marioo zaidi.

Nyimbo za Marioo

Marioo songs

Kwa sasa ameachilia nyimbo nyingi sana zikiwemo colabo na wasanii kadha. Kati ya zile nyimbo zinazojulikana ni kama vile mama Amina, ‘Bia Tamu’, ‘Chibonge’, ‘Unanikosha’, ‘Inatosha’, na ‘Ya Uchungu’. Nyimbo za Marioo huangazia halisia kama chibonge ilikuwa kwa kudhamini uwepo na uzuri wa wanawake wabonge.

Utajiri wa Marioo

Marioo ni Kati ya wasanii wanaotengeza hela zaidi kwenye mziki hii ni pamoja na mauzo ya mziki na pia performance. Utajiri wa Marioo unaasemekana kuwa zaidi ya $100,000.

Uhusiano wa kimapenzi

Hadi sasa mpenzi wa Marioo hajulikani. Inasemekana ako naye ila hajamueka hadharani. Walipofanya colabo na Jovial wengi walifikiria wawili hawa ni wapenzi ila sivyo.

Zidi kutegea hapa mwangaza news ili kuyafahamu mengi kuhusiana na wasanii wa afrika mashariki. Ni hayo tu kwa sasa kuhusiana na historia ya Marioo

Pia soma, historia ya Ibraah 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *