Historia

Historia ya professor Jay : Ugonjwa wa professor Jay

Kama utakuwa unafuatilia mziki wa bongo basi utakuwa unamfahamu professor Jay. Ni msanii aliyevuma na nyimbo yake nikusaidieJe ambapo alikuwa ameshirikiana na ferooz. Professor Jay amechangia pakubwa mziki wa bongo kusikika ulimwengu mzima. Kwa haya na mengine mengi tegea hapa mwangaza ili kuifahamu vizuri historia ya professor Jay.

Majina kamaili na mwaka wa kuzaliwa

Professor Jay ni jina la kisanii ila majina yake kamili anajulikana kama Joseph Haule. Miaka kadhaa iliyopita, professor Jay alikuwa mbunge ( Mp) wa mikumi. Professor Jay alizaliwa mwaka wa 1975, 29th December maeneo inayojulikana kama Songea nchini Tanzania.

Professor Jay alilelewa Songea alikozaliwa. Babake professor Jay aliyekuwa akijulikana kama Mzee Leonard Stephen Haule aliaga Dunia mwaka 2018 baada ya kuugua kwa mda.

Safari ya mziki yake professor Jay

Professor Jay alianza safari yake ya mziki mwaka wa 1989 akiwa chini ya band iliyojulikana kama Hard blasters. Wakati huo hakuwa anajiita professor Jay ila alikuwa akitumia jina la ” Nigga J”. Kati ya zile nyimbo zilizofanya vizuri akiwa kwa kikundi Cha hard blasters ni pamoja na “Chemsha Bongo”.

Baada ya kufanya mziki kwa mwaka mmoja, kikundi Cha hard blasters kilipata tuzo ya best hip hop group nchini Tanzania. Mwaka wa 2001, professor Jay aliamua kuachana na hard blasters na kuanza kufanya mziki kivyake. Hapo ndipo akawa mmoja wa muanzilishi wa bongo music ndani ya Tanzania.

Professor Jay alifanya collabo kadha na wasanii wenza kama vile juma nature, diamond platnumz pamoja na lady Jaydee. Collabo za professor Jay hazikuishia hapo kwani pia alivuka border na kufanya Kazi na chameleon wa nchi ya Uganda na pia akavuka Kenya na kufanya collabo na wasanii kama vile Nonini, Nazizi na Victoria kimani na hapo ndipo alitengeza jina afrika mashariki na kujulikana na wengi.

Professor Jay kwenye siasa

Joseph Haule anyejulikana zaidi kama professor Jay aliwania kuwa mbunge ( Mp) ndani ya maeneo ya Mikumi chini ya chama Cha CHADEMA mwaka wa 2015. Alipata ushindi ila mwaka wa 2020 alipoteza kiti chake baada ya kuwaninia tena kama mbunge wa Mikumi. Denis Lazaro wa chama Cha Mapinduzi ( CCM) ndiye aliyechaguliwa kuwa mbunge wa Mikumi baada ya kupata kura 31,411 huku professor Jay akipata kura 17,375.

Professor Jay ameachia album kadhaa zinazofanya vizuri na kupitia hizi nyimbo, professor Jay amepata heshima kubwa sana afrika nzima. Nyimbo zake huwa ni za mawaidha na kupitia nyimbo zake wengi hupata mafunzo.

Hizi ni Kati ya album za professor Jay

  • Machozi 2001
  • Jasho na damu 2003
  • Mapinduzi halisi 2006
  • Joseph 2007
  • Aluta continua 2014
  • Izack mangesho 2016

Afya na Ugonjwa wa professor Jay

Professor Jay hivi majuzi amelazwa hospitali na Ugonjwa ambao mpaka sasa haujawekwa hadharani. Kulingana na familia yake, msanii huyu mkongwe anaendelea vizuri na pia wametoa ruhusa kwa yeyote ambaye angependa kuchangia professor Jay ajitokeze kwani bill ya hospitili imekuwa kubwa mno na imepita uwezo wa familia

Kuna ripoti zilizotolewa kuwa professor Jay ameaga Dunia ila familia yake ilijitokeza kukanusha hizo habari na kusema kwamba professor Jay apo hai na anaendelea na matibabu. Hapa mwangaza tunamuombea professor Jay uponyaji wa haraka ili aweze kuwapatia mashabiki wake mziki mzuri. Natumai umejifunza mengi kuhusiana na  historia ya professor Jay ama ukipenda Joseph Haule. Zidi kutegea habari zetu hapa mwangaza news kwa mengi zaidi

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *