SanaaMchipuko

Historia ya Sarah Hassan Zora

Najua wengi wanamfahamu muigizaji huyu ila ni wachache wanaoijua Historia ya Sarah Hassan Zora.

Sarah Hassan ni muigizaji aliyezaliwa nchini kenya. Amewahi kuwa mtangazaji wa Tv na pia ni mwanamitindo. Katika zile tamthilia ameigiza ni pamoja na Tahidi high iliyokuwa citizen Tv na kwa sasa ni muigizaji mkuu katika tamthilia ya Zora.

Sarah Hassan ameolewa na martin dale. Sarah Hassan alikutana na bwanake Martin Dale ndani ya gym maeneo ya Westlands na hapo ndipo walianza urafiki.

Sarah Hassan husband martin Dale
Mume wa sarah hassan

Walichumbiana kwa mda mrefu alafu baadae wakafanya harusi. Harusi yao ilifanyika mwaka wa 2017 ila ilikuwa ya kibinafsi ama kwa kimombo “invites only”. Harusi yenyewe ilifanyiwa maeneo karura forest. Wawili Hawa Wana mtoto wanayempenda sanaSarah Hassan baby

 

Sarah Hassan alizaliwa mwaka wa 1988 tarehe tano September nchini kenya mjini Mombasa. Kwa sasa mrembo huyu ana miaka 31

Sara Hassan ni mtoto wa kipekee katika familia yake. Wazazi wake ni Lucian na Hassan na wote wawili ni wakaazi wa Mombasa.

Sarah Hassan parents
Harusi ya Sarah Hassan

Sarah Hassan alisomea machakos Girls High school iliyoko machakos county. Baada ya masomo ya shule ya upili, mrembo huyu aliendelea masomo yake ndani ya chuo kikuu Cha jomo kenyatta university Cha sayansi na tekinologia. Mwaka wa 2016 alielekea new york film academy kwa masomo zaidi kuhusiana na filamu ndani hollywood.

Alianza kuigiza mwaka wa 2009. Aliigiza kama Tanya ndani ya Tahidi high citizen Tv. Wakati huo, Tahidi high ilikuwa yasifika sana. Wakenya wanampenda sana kwani ana uwezo mkubwa sana katika uigizaji.

Katika zile sinema ameigiza ni pamoja na Demigods, Saints, Changes, Sakata, House of Lungula, Jane and Abel, Live or Die, Now that you’re here, Discovery +254, How to Find a spouse pamoja na Plan B.

Mwaka wa 2013, aliwahi kufanya Kazi na Noni Gathoni kwa wedding show iliyokuwa ikipeperushwa ndani ya citizen Tv. Hii show alifanya kwa mwaka mmoja na ilipofika December 2014, Sarah Hassan alijitoa. Kwa sasa ni muigizaji mkuu katika Zora Citizen Tv.

Soma hii pia ( waigizaji wa Zora Citizen Tv na majina yao kamili)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *