Siasa

Huenda Uhuru Kenyatta atamtaja Raila Odinga Kama mrithi wake

Kulingana na mambo yanavyokwenda, Kuna uwezekano rais Uhuru akamtaja Raila Odinga Kama atakaye mrithi uongozi. Kama umekuwa ukifuatilia, rais Uhuru ameonekana kumuamini sana Raila Odinga kwa kiasi kuwa anampa majukumu ya kumuwakilisha shughuli za kiserikali

Mikutano yote ya BBI inaongozwa na Raila Odinga ambapo inaonyesha uaminifu Kati ya Raila Odinga na Uhuru Kenyatta. Urafiki wa Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto unazidi kufifia na huenda ahadi yao ya Ruto kuchukua usukani ikakatizwa

Katika uchaguzi uliopita, rais Uhuru Kenyatta aliahidi kuwa akimaliza wakati wake atamwachia William Ruto Ila kwa Sasa mambo ni tofauti. Kulingana na wanasayani wa kisiasa, vitendo na maneno ya Uhuru Kenyatta zinaashiria kuwa mkaribu wake ni Raila Odinga.

Kumekuwa na mgawanyiko Kati wanainchi wa maeneo mbalimbali wengine wakiunga mkono uhusiano wao Uhuru na Raila Ila wengine wanapinga kabisa wakidai kuwa Ruto alisaidia pakubwa sana Uhuru Kenyatta kushinda uchaguzi uliopita.

Yetu ni jicho tu Ila mda ukifika tutaweza kuyafahamu yote. Maombi yetu ni amani na nchi yetu iendelee mbele.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *