Sanaa

Je, Alikiba kumtumia Hamisa Mobetto kumechangia Nini? Soma hapa

Sio wengi walitegemea alichokifanya Alikiba. Katika video yake mpya ya Dodo, Alikiba aliamua kumtumia mpenzi wa zamani wa diamond platnumz Kama video vixen. Jambo hili lilipokelewa tofauti na mashabiki, wengi wakidai Nia yake ilikuwa ni kuleta mvutano Kati ya mashabiki wake na wale wa diamond platnumz.

Kusema kweli ubunifu huu umesaidia pakubwa sana na zaidi waliotazama hii video kwa YouTube walivutiwa na Alikiba kumtumia ex wa diamond platnumz. Kwa Sasa video hiyo imefikisha milioni mbili na nusu na huenda ikapanda zaidi.

Tanasha aiaga familia ya diamond

Nyimbo yenyewe ni Kali na quality ya video imeenda shule. Kama kawaida Alikiba sio mgeni kwa hii game na utakubaliana nami kuwa anaelewa anachokifanya. Japo yeye hukaa mdaa mrefu kabla ya kuachia nyimbo, nyimbo zake hukaa kwa mda mrefu kwa maskio ya watu na kila Mara unaposkiliza nyimbo hizi unahisi Kama ni mpya.

Je, unafikiri Alikiba alifanya kusudi kumtumia Hamisa Mobetto ama alimtumia Kama vile msanii mwingine angefanya tu. Tupia maoni yako hapa chini ili tuweze kupata jibu.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *