Mchipuko

Je, Ni kweli tanasha alikataa kuwepo kwa video ya diamond platnumz, naanzaje?

Kwa wale wamekuwa wakiuliza kama Je, Ni kweli tanasha alikataa kuwepo kwa video ya diamond platnumz, naanzaje? Jibu tunalo hapa mwangaza news

Tanasha Donna amefunguka kwamba alikatalia diamond platnumz ombi lake la kuwa kwa video ya ” Naanzaje“. Director wa video ya Naanzaje yake diamond almaarufu kama hanscana pia alieleza mashabiki kwamba diamond platnumz alitaka sana tanasha awe kwa video yake.

Tanasha Donna

Kulingana na hanscana, diamond platnumz alimpigia tanasha ili kumuomba awe kwa video yake kama video vixen ila tanasha akakataa katakata japo mwanzo alitaka apewe mda afanye uamuzi. Baada ya mda tanasha alitoa jibu lake kwa diamond platnumz na kumwambia hawezi kuwa katika hiyo video.

Bado haijajulikana aliyemshauri tanasha Donna kutokubali ombi la diamond ila inasemekana lazima kutakuwa na mshauri aliyemkataza tanasha Donna kuwa kwenye hiyo video.

Kulingana na Kiss 100, waliweza kuwasiliana na tanasha Donna ambaye alikubali kuwa uvumi huo ni wa kweli. Hakutaka kuongea mengi kuhusiana na Jambo hilo ila alikubali kuwa alikataa wito wa aliyekuwa mume wake diamond platnumz.

Tanasha huenda akaachia Ep yake mpya karibuni na juzi alikuwa amekutana na Alikiba ndani ya Trade mark hotel kwenye tamasha ya listening party ya Alikiba

Tarehe mbili October tanasha aliandaa sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa mwanawe naseeb junior. Hii ni shrehe ya pili na naseeb junior kwani saa hii ako na miaka miwili.

Naseeb junior birthday

Tanasha alipachika picha ya naseeb junior kwenye Instagram page yake na kuandika meseji ya kuvutia kwa mwanawe;

“Mnamo tarehe mbili October, miaka miwili iliyopita, mfalme alizaliwa. Nakutakia siku njema ya kuzaliwa mtoto wangu. Nakupenda kupindukia na sijui vile maisha yangu yanaweza kuwa bila wewe. Uwepo wako unayafanya maisha yangu yawe kamili. Mola azidi kukulinda na ayape maisha yako muongozo mzuri. Mama anakupenda na wewe ni baraka kwangu…”

Naseeb junior walizaliwa siku moja na Babake ambaye ni diamond platnumz Ina maana wanasherehekea birthday yao siku moja. Upande wa diamond platnumz siku ya kuzaliwa kwa naseeb junior, alipost picha ya mtoto wake bila kueka neno kwa post yake.

Mamake diamond almaarufu kama mama dangote alisherehekea birthday ya mjukuu wake na kueka haya maneno kwenye Instagram page yake;

“Tom kama Tom lakini kaka maisha marefu Babu bibi anakupenda sana sana Naseeb kichwa pacha wa Naseeb Simba…”

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *