Mchipuko

Je, Tanasha na Jamal Gaddafi wako kwenye uhisiano?

Aliporudi nchini kenya, Tanasha Donna amekuwa kwa ukaribu sana na mtangazaji wa runinga ya KTN Jamal Gaddafi. Wengi wamekuwa wakiwafuatilia ili waweze kujua kama kweli wawili hawa wako kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Jamal ndiye alikuwa wa kwanza kueneza habari za Tanasha Donna kubadili dini na kuwa muisilamu. Aliweza kualika Tanasha Donna kwenye familia ya uisilamu. Kama unakumbuka vizuri mwanadada huyu alibadilisha jina lake la ki kristo na kwa sasa anajulikana kama Aisha.

Jamal Gadaffi and Tanasha

Tokea siku hiyo wawili hawa huonekana pamoja hata siku chache zilizopita walipatikana Eastleigh ambapo inasemekana huwa wanawasaidia¬† watoto mayatima kwa kuwapa msaada huko Eastleigh children’s home. Kwa sasa Tanasha donna anasemekana kuwa na kampuni yake inayojulikana kama Tanasha Donna community home yenye inasemekana kuwa chini ya usimamizi wa Jamal Gaddafi.

Jamal Gadaffi and Tanasha and some muslims friends

Katika mahojiano yake na Mzazi willy Tuva ndani ya Radio citizen, Tanasha alisema Gaddafi sio mpenzi wake ila ako kwa timu yake na anamsaidia tanasha mambo madogomadogo.

Namjua vizuri na yeye ni kama kakangu. Dadake pia ni rafiki yangu na tunajuana vizuri kwa hivyo hatupo kwenye uhusiano na Jamal.

Soma hii pia (Teacher Wanjiku aamua kufuata Nyayo za Babu Owino)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *