Mchipuko

Jinsi ya kulipia king’amuzi Cha Azam

 

Jinsi ya kulipia king’amuzi Cha Azam

Wengi wangekuwa wakitaka kujua Jinsi ya kulipia king’amuzi Cha Azam. Kumbuka Azam Ina chaneli mbalimbali zikiwemo za burudani, habari na sports.

Ningependa mwanzo kukujuza Jinsi ya kulipia king’amuzi Cha Azam ukitumia mtandao wa Airtel. Unachotakiwa kufanya ni bonyeza *150*60# kwenye simu yako alafu Bonyeza 5 (lipa bill) kisha Bonyeza 2 itakayokupatia orodha, Bonyeza 1 – TV Ving’amuzi.

Pia kuna wengi wameulizia Jinsi ya kulipia king’amuzi Cha Azam sports ili uweze kupata chaneli Kama vile Azam Sports HD na vilevile, njia ya kubadilisha vifurushi kama utakuwa unahitaji kifurushi tofauti na ulichokilipia. Nitakupa utaratibu wa kufanya haya yote na naomba uweze kuwa makini na maelezo haya na bila shaka utafaulu. Kumbuka hii ni wakaazi wa Tanzania wanatumia Ving’amuzi vya Azam.

 

Azam iko na vifurushi vinne vikuu na wengi wanavielewa ila pia unaweza pata nyongeza ya vifurushi continue viwili. Orodha ya vifurushi hivi vikuu ni Kama ifuatayo;

Azam Pure ambayo ni 12,000

Azam plus ambayo ni 20,000

Azam play ambayo ni 25,000

Kihindi pekee pia waweza pata kwa Bei ya 16,000

Pia katika vile vifurushi viwili vya nyongeza ni Kama vile Azam sports 15,000 na moja ya kihindi Bei yake ikiwa 6,000.

Jinsi ya kulipia king'amuzi Cha Azamsport HD

Kwa wale wangependa kupata Azam sports HD, unatakiwa uwe na kifurushi nyongeza za Azam sports ambacho gharama yake ni Elfu kumi na tano. Wacha tuseme kwa mfano uko kwao kifurushi Cha Azam Pure, basi unatakiwa kulipa kiwango Cha Elfu ishirini na saba. Yaani 15,000 + 12000.

Kama uko kwao Azam plus basi utalipa 20,000 + 15,000 ambapo ukijumuisha itakuwa 35,000 ukiwa na Azam play basi utalipa jumla 40,000 ( 25,000 + 15,000)

Utaratibu wa Jinsi ya kulipia king’amuzi Cha Azam sports;

1. Fanya malipo ya shilingi 15,000 na kisha piga namba *150*50*5#

2. 2. Chagua namba 3, Sajili Huduma Mpya.

3. 3. Ingiza namba ya smartcard.

4. 4. Chagua namba 6, Azam Sports Add on 15,000

5. 5. Baada ya hapo subiri dakika 5-20 utapata chaneli.

Kama umefungiwa kifurushi chako na unataka Azam Sports HD pia;

1. KABLA ya kufanya malipo, piga namba *150*50*5# kwanza.

2. 2. Chagua namba 3, Sajili Huduma Mpya.

3. 3. Ingiza namba ya smartcard.

4. 4. Chagua namba 6, Azam Sports Add on 15,000

5. 5. fanya malipo ya jumla ya kifurushi chako kikuu na cha Azam Sports HD pia. Kwa mfano lipia jumla ya shilingi 27,000 kama ulikuwa una kifurushi kilichofungiwa cha Azam Pure na unataka cha Azam Sports pia. Yaani 12,000 + 15,000 = 27,000. Vile vile fanya kujumlisha ulichonacho sasa kama ni tofauti na Azam Pure.

6. 6. Baada ya hapo subiri dakika 5-20 utapata chaneli.

Kama umefungiwa na unataka kubadili kifurushi cha sasa na kuongeza cha Azam Sports pia;

1. KABLA ya kufanya malipo, piga namba *150*50*5# kwanza.

2. 2. Chagua namba 2, Badilisha Kifurushi

3. 3. Ingiza namba ya smartcard

4. 4. Chagua kifurushi

5. 5. piga namba *150*50*5# tena

6. 6. Chagua namba 3. Sajili Huduma Mpya

7. 7. Ingiza namba ya smartcard

8. 8. Chagua namba 6 Azam Sports Add on 15,000

9. 9. Fanya malipo ya jumla ya kifurushi chako kikuu na cha Azam Sports HD pia. Kwa mfano lipia jumla ya shilingi 27,000 kama ulikuwa una kifurushi kilichofungiwa cha Azam Pure na unataka cha Azam Sports pia. Yaani 12,000 + 15,000 = 27,000. Vile vile fanya kujumlisha ulichonacho sasa kama ni tofauti na Azam Pure

10. 10. Baada ya hapo subiri dakika 5-20 utapata chaneli

Kama ulishalipia lakini unataka kubadili kifurushi kikuu, fanya hivi;

1. Unaruhusiwa kubadili kifurushi kikuu ndani ya siku mbili baada ya malipo kwa kuongezea tu malipo yako. Kama zimepita siku mbili, LAZIMA ulipie upya kifurushi hicho.

2. 2. Kisha Piga *150*50*5#

3. 3. Chagua namba 2, Badilisha Kifurushi

4. 4. Ingiza namba ya smartcard

5. 5. Chagua kifurushi

6. 6. Baada ya hapo subiri dakika 5-20 utapata chaneli.

Tazama hii pia ( video mpya ya Mbosso, Fall )

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *