Mchipuko

Kama una miaka zaidi ya hamsini huezi elewa Mziki wangu, Harmonize asema

Baada ya kuachia album yake ya highschool, harmonize amekuwa akipata maoni tofauti kwa kila anayeisikiza album hiyo.

Wengi wasema album yake haieleweki huku wengine wakimkosoa kwa kutumia kizungu mingi kwa nyimbo zake kadhaa. Album ya highschool iliachiliwa kama miezi miwili iliyopita na harmonize anaendelea kuifanyia marketing zaidi.

Kupitia insta story, Harmonize amewapa makavu wanaokosoa album yake akidai labda miaka yao haiwaruhusu kuelewa mziki wake. Kulingana na yeye, mziki wake ni wa watu wenye chini ya miaka hamisi. Harmonize amesema kwamba Nia yake ni kubadilisha mziki wa afrika mashariki.

Album ya highschool yake harmonize Ina utofauti sana na mziki wa Tanzania na labda ndio maana wengi hawajamuelewa kabisa. Ni hivi majuzi baba levo aliikisoa album hiyo na kumtaka harmonize kurudi studio ili arekodi album nyengine na achane na hii album ya highschool.

Je wewe unaweza sema nini kuhusiana na hii album ya harmonize? Unadhani amefanya Kazi nzuri ama kachemsha. Zidi kutegea hapa mwangaza news kwa mengi zaidi.

Tazama video ya harmonize outside hapa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *