Sanaa

Kutana naye Bigsoul, mhandisi wa sauti katika tamthilia ya pete

Anajulikana Kama Alex Mugenda Ila wengi wanamfahamu Kama bigsoul. Gwiji huyu ametokea jijini Nairobi japo pia ana familia mkoani pwani. Alianza kutayarisha mziki miaka kadhaa iliyopita na aliweza kufanya nyimbo nyingi tajika Kama vile “my city my town” yake prezzo na canibal.

Kama unawakumbuka camp Mulla basi utakuwa unamfahamu zaidi. Bigsoul Ana talanta zaidi ya moja kwani yeye pia ni mwanamziki na pia mwalimu wa mziki. Kwa hivi Sasa ameingia katika kitengo Cha filamu na kwa kweli anakifahamu anachokifanya.

Kama umekuwa ukifuatilia tamthilia ya pete na umekuwa ukipendezwa na mziki unaocheza pale, Basi fahamu kuwa ni mkono wake gwiji huyu. Kwa Sasa tamthilia ya pete imepata umaarufu zaidi nchini Kenya na nchi jirani ya Tanzania.

Kiongozi wa filamu hiyo Daudi anguka alinukuliwa akisema kuwa tamthilia hii itaendelea kwa mda Ila pia anajitayarisha kuachia kazi zaidi. Inasemekana Daudi Anguka ni mmoja wa wakurugenzi walio na umri mdogo katika kitengo Cha filamu.

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *