Sanaa

Lukamba aingia na wake wawili kwenye tamasha la Zuchu

Ukimuuliza Lukamba kama angependa wake wawili ama mmoja, basi jibu lake litakuwa bibi wawili. Lukamba ni mpiga picha rasmi wa diamond platnumz.

Juzi katika show ya Zuchu iliyoandaliwa na wasafi, Lukamba aliamua kuingia na bibi wake wawili kwenye tamasha hiyo.

Lukamba ana mtoto mmoja na kama wiki mbili zimepita alifunga pingu za maisha na bibi wake wa pili na aliamua kutoka na wawili hao kwa wakati mmoja.

Alipofika kwenye Hilo tamasha, aliamua kupiga picha na wawili hao huku akimpa kila mmoja sifa tele.

Wakwanza kumtambulisha kwa red carpet alikuwa bibiye wa kwanza Shuu Mimi aliyevamilia nguo ya rangi ya dhahabu. Na kama ilivyo desturi kwa wanaume wengi, Lukamba alimchukulia mke wake wa kwanza kama malkia.

Wawili hao walipiga picha kadhaa pamoja kabla hajaenda kumchukua mke wake wa pili ambaye ni miss teen heritage Tanzania. Ceceey ambaye ni mke wa pili wa Lukamba alivalia nguo nyeusi ilioonyesha maumbile yake.

Kwa Instagram yake, Lukamba akimsifia mke wake wa pili kuwa ni mwaminifu na mtiifu

Soma hii pia ( princess Tiffah azidi kushangaza wengi)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *