Mchipuko

M.C.A apinga vikali uamuzi wa Gavana Joho kuhusu Corona virus

Masaa kidogo tu baada ya gavana wa county ya Mombasa Hassan joho kupiga marufuku vilabu vya usiku, Kitula ambaye ni M.C.A wa freretown hakufurahishwa na uamuzi huo. Kitula alisema kuwa serikali kuu haijafikia uamuzi huo kwa hivyo pia viongozi wa county ya Mombasa hawana mamlaka hayo.

Kitula aliongezea kuwa kufunga sehemu za starehe itazidi kudhuru uchumi na pia itaumiza wanabiashara wanaotegemea hiyo biashara. Juzi katibu wa wizara ya afya alitangaza kuwepo kwa virusi vya Corona Ila alihimiza wakenya wasiwe na wasiwasi kwani serikali na wizara ya afya wamejihami vilivyo

Matamshi ya Kitula yalipokelewa na hisia tofauti kwani wanainchi waliweza kuchangia wengi wakiunga Kitula mkono na wengine wakidai Hana ufahamu wowote kuhusiana na Corona virus na uongozi wa county ya Mombasa hivyo anafaa kuachia gavana wa county hiyo mamlaka ya kuamua.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *