Afya

Maelezo mafupi kuhusu nguvu za kiume

Nguvu za kiume ni uwezo wa mwanamume kukamilisha tendo la ndoa. Mara nyingi uume unashindwa kusimama na kumnyima nafasi mwanaume kufurahia tendo la ndoa na mwanamke ampendaye na hata kuzalisha watoto.

Tatizo hili hutokea kwa asilimia kubwa sana ya wanaume japo wengi hushindwa hata kusema kwa daktari ili wapate matibabu.

Dawa ya nguvu za kiume

Wengi wamekuwa wakiulizana je, tatizo la nguvu za kiume lina tiba? Kuna uwezekano mkubwa sana wa kupona tatizo hili kupitia dawa za kienyeji na dawa za kemikali. Kulingana na watibabu wa kienyeji, kitunguu saumu ni dawa ya nguvu za kiume.

Ni mhimu sana kuhakikisha kwamba chakula unachokipika kimetayarishwa na viungo kama vile kitunguu saumu kwani kitunguu saumu ni mojawapo ya dawa ya nguvu za kiume.

Endapo unataka dawa ya kiume ya haraka, unatakiwa kutembelea mtaalamu. Uzuri wa kumhushisha mtaalamu ni kwamba, kabla ya matibabu yake, atafanya vipimo ili aweze kubaini tatizo lako na chanzo kuu ya hali yako.

Unafaa ufahamu kwamba, tatizo la nguvu za kiume linatibika na unachotakiwa kufanya ni kuwa muwazi ili uweze kusaidika. Kumbuka mficha uchi hazai.

Hizi ndizo njia zinazopunguza nguvu za kiume

Uvutaji wa sigara

Najua wengi washawahi kuona onyo kwenye pakiti za sigara. Wengi huwa wanaona kuwa onyo hii haina uzito wowote Ila kwa kweli uvutaji wa sigara unachangia kupungua kwa nguvu za kiume. Kumbuka sigara pia zinaleta magonjwa sugu kama vile saratani ya Koo na hata mapafu. Kulingana na utafiti, wengi wanaovuta sigara hulemewa na tendo la ndoa.

Kuvaa suruali zinazobana

Wanaume wengi hupenda kuvaa nguo za kubana wakidai ni fashoni. Kusema kweli hawajui madhara wanayoyafanya kwa sehemu zao za Siri. Mayai ya mwanaume huwa yatakiwa kupumua na pia kupata nafasi ya kuzunguka. Unapovaa nguo za kubana huwa unayanyima mayai nafasi ya kuzunguka. Mayai ya mwanaume yasipopata nafasi hio huenda yakafa ama kukosa nguvu za kuogelea.

Ukunywaji wa pombe.

Pombe Ina starehe zake Ila unapokunywa zaidi inakuwa sumu. Unafaa unywe pombe kwa vipimo la sivyo utashukisha uwezo wako wa kutenda to tendo la ndoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *