Mchipuko

Magufuli ahimiza wanaotoa barakoa za bure wakamatwe

Kuvaa barakoa kumekuwa mtindo wa kila siku. Kifaa hichi kinavaliwa karibu na kila mtu siku hizi na kama unakumbuka vizuri, madaktari na wahudumu wa hospitali ndio waliokuwa wakivaa sana kifaa hiki hapo awali.

Ni juzi tu Dr. Pombe Magufuli aliwahimiza wakulima wapandishe bei ya chakula yao wakataki wanauzia nchi za Kigeni. Magufuli alisema nchi hizo ziliwafungia wanainchi wao badala ya kuwaruhushu kufanya kazi. Rais Magufuli mpaka sasa hajawahi fungia nchi yake eneo hata moja. Kulingana na yeye, hawezi kufungia wanainchi maana wanatakiwa wapate chakula chao cha kila siku na pia akiwafungia, uchumi wa nchi utazorota.

Magufuli jana amesema kuna kikundi kinajiita Magufuli forum kinachozunguka huku kikipeana Barakoa za bure. Amesema hatakubali jambo hilo kwani barakoa hizo hazijadhibitishwa na kituo cha afya nchini tanazania. Amewahimiza wanainchi wajihadhari sana maana barakoa hizo hazijulikani zimetoka wapi.

Barakoa Mask

Amewahimiza watanzania waendelea kumuomba Mungu kwani yeye ndiye tegemeo. Kanisa na misikiti nchini humo bado zipo wazi na ibada zinaendelea kama kawaida. Mataifa mengi wamekuwa wakimpinga Magufuli kwa uamuzi wake ila yeye hajalegeza kamba. Kwa sasa watanzania wengi hawavai barakoa na shughuli zinaendelea kama kawaida tofauti na nchi zingine.

Tazama hii video

Soma hii pia (Tazama mkewe George Floyd alivyojawa na machozi wakati wa mazishi ya mmewe)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *