Maisha

Maisha ya Muthoni wa Kirumba

Mtangazaji mashuhuri Muthoni wa Kirumba asema alikuwa mtukutu akiwa shule. Aliwahi kufukuzwa kwa uuzaji na usambazaji wa madawa na pia kuvunja sheria za shule.

Katika mahojiano yake ndani ya youtube wakiwa na Dan Wainaina, alisikika akiwashauri wanafunzi wawe na tabia nzuri shuleni kwani utukutu haulipi.

Katika mahojiano, Muthoni wa Kirumba alieleza tukio ambalo alipigana natangazaji mwenza Keziah Kariuki matangazo yao yakiwa Live. Hii ilichangia wawili hawa kusimamishwa Kazi kwa mda

Former Kameme TV presenter Keziah wa Kariuki
Keziah Kariuki

Kulingana na Muthoni Kirumba, alipata habari kuwa Keziah Kariuki alikuwa akisambaza uvumi kwamba Muthoni Kirumba anauza madawa ya kulevya na pia ni mtumiaji. Ndipo siku moja wakiwa kwa show yao wakati wa mapumiziko wawili hawa waliamua kupimana nguvu.

” Wakati tupo on air niligundua mwenzangu Keziah Kariuki ananichokoza ndio nikaamua kujitetea, wakati mziki unaisha nilimzaba Kofi kwani alikuwa yuaniongelesha vibaya.

Muthoni Kirumba alipumzishwa wiki mbili huku mwenzake Keziah Kariuki akipumzishwa wiki moja. Muthoni aliongeza kuwa hata leo bado ako na barua yake Ila yeye na Keziah Kariuki ni marafiki kwa sasa.

Muthoni wa Kirumba Kameme FM

Baada ya mapumiziko, wawili hawa walirudi kazini na kuendelea kufanya Kazi pamoja huku uhusiano wao ukirudi sawa. Tokea enzi za hapo nyuma, Muthoni wa Kirumba alionekana mwanadada aliyesumbua sana nyakati za shule kwani pia aliwahi kumpiga mshauri aliyekuwa akiwahutubia shuleni mwao kuhusiana na mambo na elimu.

Kulingana na yeye, mshauri huyo ni kama alikuwa anaongelea maisha yake.

” Nikiwa shule nilikuwa nakuza mboga aina ya Kabichi la Kukaanga kwani nilikuwa nasoma masomo kuhusiana na ukulima”.. nilibeba Kabichi la Kukaanga na wakati wa Maombi nilisimama nyuma ya yule mshauri na kumgonga nalo…”

Kulingana na Muthoni Kirumba, yule mshauri aliona kama amevamiwa kwani hakudhania Jambo kama lile lingetokea. Kwa sasa wawili hawa ni marafiki kwani walikutana na wakasameheana japo Muthoni Kirumba alipewa adhabu humo shuleni.

Muthoni wa Kirumba anamshukuru Babake kwa maana bali na utukutu wake, Babake haikuwahi kumuacha na alimpa elimu mpaka akamaliza masomo yake. Kwa sasa Muthoni wa Kirumba anafanya show na kihenjo ndani ya Kameme Fm inayojulikana kama Cajamuka.

Soma hii pia : Historia ya kihenjo

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *