Maisha

Maisha ya Stivo Simple Boy yazidi kunyooka

Wakati Stivo Simple Boy ( Ndio Manaake) alipoachia nyimbo yake ya kwanza, wengi walimcheka Sana wakisema kuwa hawezi enda mbali wakidai nyimbo zake hazina maana yoyote. Wengi walimfananisha na mnyama flani lakini kwa hivi sasa itabidi wajifiche maana Stivo Simple Boy ako kiwango kingine.

Stivo Simple Boy girlfriend

Sio wote waliomuonea gere, kuna watu walimuombea mungu ili aweze kufanikiwa maishani. wengi walimtakia mafanikio ndio aweze kuisaidia familia yake iliyosimama na yeye wakati mgumu. Mungu aliyasikia maombi ya wengi na kwa sasa Stivo Simple Boy anaishi maisha mazuri kwa sasa.

Stivo Simple Boy hakuwasikiza waliomkashifu na aliamua kubidiika. Jina lake liko juu afrika mashariki na kwa sasa wengi wanamfahamu. Kwa sasa anapata dili kubwa na maisha yake yamebadilika sio yule Stivo Simple Boy wa “Ndio Manaake”.

Juzi kwenye Instagram page yake aliweka video akijifundisha mchezo wa skateboard. Huu mchezo hufahamika zaidi kwa familia matajiri ila kwa sasa Stivo simple boy aliyelelewa maghettoni anacheza michezo ya matajiri.

Wengi walipoitazama hii video walionekana kufurahia maendeleo ya Stivo simple boy na kumuombea azidi kufanikiwa maishani.

Tazama (video mpya ya willy Paul)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *