Maisha

Maisha ya Terryanne Chebet baada ya kusimamishwa kazi citizen Tv

Terryanne Chebet ambaye alikuwa alifanya kazi Citizen Tv amefunguka na kueleza aliyoyapitia baada ya kupoteza kazi ndani ya citizen Tv inayomilikiwa na royal media. Ameamua kufunguka ili kuwasaidia na ushauri wanahabari waliopoteza kazi kwa media tofauti ikiwemo NTV na K24TV.

Terryanne Chebet alisema kwamba, aliposimamishwa kazi katika kampuni ya royal media, alijihisi mnyonge na mwenye hasira. Hii ilimfanyikia mwaka wa 2016. Jambo hili lilimshtua sana kwani hakujua la kufanya.

Lakushangaza ni kwamba, Chebet alisimamishwa kazi lisaa limoja kabla ya kuingia ndani ya studio ili kutayarisha kipindi chake cha Business centre.

” Hii ilikuwa siku ya huzuni kwangu, nakumbuka nililia usiku kutwa,sikujua nifanye Nini.. baadae nilijipa moyo na nikaamua kupambana na hali yangu… Niliamua kusahau yote na kuamua kujenga yajao kwani nilikuwa na familia iliyokuwa inanitegemea…”

Aliwasihi wenzake walizopoteza kazi nation Media group na Royal media services wachukue mfano wake ndio waweze kujikusanya tena ili waendelee na maisha yao.

Terryanne Chebet aliamua kugeuza mipangilio yake ya vile alikuwa anatumia pesa kwa kupunguza mahitaji mengine ili aweze kukidhi mahitaji yake ya kila siku.

Kulingana na mwanadada huyu, aliweza kunakiri mahitaji mhimu na kufanya hesabu ya pesa anayoitumia kama vile nauli, Kodi na chakula ili aweze kufahamu vile anatumia pesa zake.

Aliweza kupunguza matumizi mengine yenye hayakuwa ya lazima kama vile kula chakula nje na vinywaji. Aliamua kutumia pesa yake kwa mambo mhimu tu na kupunguza mahitaji mengine.

terryanne Chebet

” Kabla ya kusimamishwa kazi, Mimi na familia yangu tulikuwa na tabia ya kula chakula Cha nje kila siku ya jumapili. Hii ilibidi niwache na niliweza kuelezea familia yangu uamuzi huo na uzuri waliweza kunielewa…”

Terryanne Chebet aliwashauri wanahabari wenza waweze kuchukua bima ya afya kwa familia nzima kwa jumla ili chochote kile kikifanyika kinachohusiana na afya ama magonjwa, waweze kujikimu. Aliongezea kuwa ni mhimu pia kulipa (NHIF) nation health insurance fund.

“Pia ni vizuri kuweka pesa kwa benki kama utapata mapato yoyote. Kama unapata kiwango flani, jifundishe kugawanya hizo pesa na hakikisha umehifadhi kiwango flani itakayo kusaidia kwa maisha yako ya baadae.. hii yaweza kuwa kila wiki ama kila mwezi..”

“Sio lazima ufanye kazi ya utangazaji, kuna watu wengi nawajua wanapika keki na baada ya kuuza wanapata pesa nyingi. Kwa hivyo wakati kama huu nawashauri wenzangu waweze kufikiria Aina ya biashara watakayoifanya kabla ya kupata kazi ya utangazaji sehemu nyengine tofauti” alisema terryanne Chebet.

Soma hii pia ( video mpya ya diamond platnumz na Rayvanny)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *