Mazishi ya kiisilamu

  • Mazishi ya kiisilamu
  • Kuzikwa kwa heshima kwa dini ya kiisilamu.

Nimepokea maswali kutoka Kwa nduguzangu wakristo kuhusu taratibu za mazishi ya kiisilamu

Kwa kawaida Kwa waisilamu, maiti kusafirishwa huwa sio Jambo la lazima Sana Kwani Mtu huzikwa popote pale mauti yatakapo mkuta ,waeza shangaa mwendazake Haji kuzikwa kwenye maava ya Uma ambapo kwao garisa angesitiriwa vyema.mara nyingi mazishi yetu hutegemea na majira ya saa za ibada ukizingatia huwa tuna swali mara 5 Kwa siku

kumuombea maiti

Fajir 5 am

Dhuhur 1pm

Alasir 4pm

Magharb 6pm

Ishai 8pm

Mara nyingi mazishi hufanyika kuanzia saa Saba Hadi sakumi mcha ili kusubiria watoto ama familia ilioko karibu kufika huwa hatupendelei kufanya mazishi usiku ispokuwa Kwa dharura ama awe mwendazake alikufa Kwa ajali na kupelekea mwili wake kuharibika vibaya ambapo hulazimu mwili wake uzikwe mara moja .

Taratibu zote za mazishi hufanyika nyumbani Kwa mwendazake ama msikitini “Ghusul” kuoshwa Kwa maiti huwa lazima kabla ya ibaada ya swala ya maiti ama” salat janaza”waisilamu huwa hawazikwi na jeneza Bali hutumia nguo maalum yakuzikia (sanda)ambayo hutumika Kwa waisilamu wote pindi Tu mmoja wao atakapo fariki.

hukumu baada ya kufa

Msikiti wetu wa mashariki cha(South c)tulifanya mataarisho kikamilifu na baadhi ya miskiti mjini Mombasa pia watu walijumuika Kwa ibada za wafu,imekuwa kama desturi inchini Kenya kwamba endapo mmoja wetu atapatwa na umauti basi nijukumu lako kumshuhulikia kama muisilamu mwenzako Kwani waisilamu wote ni ndugu hio huleta picha nzuri machoni mwa watu. Hii ilianzishwa marsabit Kwani waisilamu waliokuwa wameaga dunia Kwa ajali za Barbarani hususan ya moyale kuelekea Ethiopia wamekuwa wakizikwa huku bila kujali anatokea wapi ama kuelekea wapi ilimradi ni muisilamu basi angepewa heshima yake na kuzikwa

Itakapofikia maiti ashataarishwa basi hufungwa na kipande cha sanda ambacho bei yake huwa chini ya shilingi 500.

Kufikia hapo mwili huingizwa kwenye jeneza nakupelekwa msikitini ,huekwa nyuma kabisa ndani ya msikiti na kusubiri ibada zakawaida kuanza.

Baada ya Ibada kuisha huekwa tangazo kujuza wauimini kuwa kuna mwendazake aidha  mume ama mwanamke na yeyote ambae angependa kubaki na kujumuika ruhusa .

Baada ya hapo jeneza huletwa mbele kabisa Kwa ibada maalaum mtoto ama mmoja wa familia husimama nakuuliza jumuia endapo kuna mtu aliekuwa anamdai marehu ama ana deni lake alipwe ,baada ya hapo watu wote husimama nyuma ya jeneza na imam huongoza ibada ya wafu,wakati mwengne hutokea kukawa na maiti wa wili basi wote hulazwa Kwa mpangilo Kwa pamoja ,ibada huchukua takribani dakika 10,wanapo maliza mwili hubebwa na vijana ambao mara nyingi huwa hawajuani na marehemu

Pindi tu jeneza litakapo fikishwa kaburini basi baadhi ya familia huchaguliwa mtoto ama ndugu wa marehemu huingia kaburini ambalo huwa limeshataarishwa lakini pia huwa twatengeza mto Kwa kutumia udongo ili kueka kichwa cha marehemu.

Baada ya kuutoa mwili kutoka kwenye jeneza basi huulaza moja Kwa moja kwenye kaburi Kwa ubavu wake wakulia tukiwa tumeelekeza kichwa chake kibla (Mecca)Kwan wauimini wote wakiisilamu huangalia makah wakati wa kuswali.

Mbao huletwa na kufinikwa juu ya mwanandani yaani pahali alipolazwa maiti alafu udongo uliochanganywa na maji huletwa ilikufinika sehemu za wazi.

Soma hii pia ( ndoto za nyoka na maana yake)

Watakapo maliza hutoka nje ya kaburi na michanga huanza kumwagwa ndani ya kaburi ,watu wengi hupokezana Kwa zamu kutupa michanga kaburini wanaojulikana na wasio julikana hujumuika pamoja kwenyeshughuli hio

Baada ya shughuli za ufukiaji kuisha hutuba ama ukumbusho hutolewa ambao huchukua dakika 5 Hadi 10 hakuna maoni ama Sheria baada ya kuzika sio kaburini wala msikitini sote huwa Sawa .

Wanawake hawaruhusiwi kufika kaburini na kama watafika basi watashudia Kwa umbali tu.wanaume hubeba vyombo vilivyotumika na kuviregesha vipasavyo kuwekwa familia hubaki nyuma Kwa maombi zaidi.

Shughuli yote ya mazishi huchukua Muda WA dakika 30 na huwa kilakitu kimeisha.

Endapo kama ntakua nmesahau kitu chochote mungu ndie mjuzi wa kilakitu

Ninaimani haya machache yatakufunza kuhusu Imani yetu ya uisilamu

Soma hii pia ( jinsi ya kuoga janaba)

 1,020 total views,  1 views today

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *